YULE mchezaji aliyeng'atwa meno na Luis Suarez kwenye Kombe la Dunia, Giorgio Chiellini usiku wa jana amefunga mabao yote matatu peke yake, Italia ikiilaza Azerbaijan 2-1 katika mchezo wa Kundi H kufuzu Euro The Azzurri wakiendelea vizuri chini ya kochampya, Antonio Conte.
Azerbaijan 'walipaki basi' wakicheza na
walinzi 10 na Italia ikapata tabu sana
kuupenya ukuta wao hadi Chiellini
alipotumia makos a ya kipa kuipa Azzurri bao la kuongoza dakika ya 44.
Chiellini akajifunga kuisawazishia Azerbaijan dakika ya 76 katika harakati kuokoa mpira wa kona- lakini bahati nzuri akasahihisha makosa yake kwa kuifungia Italia bao la ushindi
dakika ya 82. katika mechi nyingine za Kundi H, Croatia imeifunga 1-0 Bulgaria bao pekee la Nikolay
Bodurov la kujifunga dakika ya 36 na Norway imeifunga 3-0 Malta, mabao ya Moeller Daehli dakika ya 22 na Joshua King dakika ya 26 na 49.
Chapisha Maoni