0
NAHODHA Robin van Persie ameifungia
Uholanzi ikipata ushindi wa kwanza katika mechi tatu chini ya kocha Guus Hiddink tangu arithi mikoba baada Louis Van Gaal, baada ya kuifunga Kazakhstan mabao 3-1 katika mechi ya Kundi A kufuzu Euro 2016.
Kazakhstan walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Rinat Abdulin dakika ya 18 kabla ya Klaas-Jan Huntelaar kusawazisha dakika ya 62.
Wageni walipata pigo baada ya mchezaji wao, Bauyrzhan Dzholchiev kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumchezea rafu Ibrahim Afellay dakika ya 64.
Afellay akaifungia Uholanzi bao la pili dakika ya 82 kabla ya Robin van Persie
‘kuunenepesha’ ushindi kwa bao la dakika ya 89 kwa penalti. Katika mechi nyingine za Kundi A, Iceland imepata ushindi wa ugenini wa 3-0 dhidi ya Latvia na Jamhuri ya Czech
imeshinda ugenini pia 2-1 dhidi ya Uturuki.

Chapisha Maoni

 
Top