MABAO ya Mohamed Elneny na Mohamed Salah yameipa Misri ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Botswana katika mchezo wa Kundi G kufuzu AFCON mwakani nchini Morocco uliofanyika jana usiku.
Mafarao ambao walipoteza mechi zao mbili za kwanza za kundi hilo mbele ya Senegal na Tunisia mwezi uliopita, wamerudi barabarani baada ya ushindi huo. Timu hizo zitarudiana
mjini Cairo Jumatano.
Katika mechi nyingine za jana, Senegal na Tunisia zimetoka sare ya bila kufungana kama ilivyokuwa kwa Lesotho na Angola.
Mechi za kufuzu AFCON zinatarajiwa
kuendelea leo, Guinea ikimenyana na Ghana mjini Conakry mchezo wa kundi E, Sierra Leone na Cameroon Kundi D,
Uganda na Togo Kundi E, Malawi na Algeria, Ethiopia na Mali, Msumbiji na Cape Verde, Kongona Afrika Kusini, DRC na Ivory Coast, Niger na Zambia, Sudan na Nigeria na Gabon na Burkina Faso.
Chapisha Maoni