Kamati ya ufundi inayoshughulikia Oganizesheni ya Mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania (UKAWA) imeandaa mkutano wa
hadhara unaotarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Singo Benson Kigaila amesema tayari wamesha fuata taratibu zote za kufanyika kwa mkutano huo wa hadhara
ikiwemo kulitarifu jeshi la polisi na kwa kupitia mkutano huo UKAWA watatoa msimamo wao juu ya katiba pendekezwa.
Kigaila amesema viongozi wa UKAWA watatumia fursa ya mkutano huo pia kuelezea namna vyama
hivyo visivyoridhishwa na maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi
wa 12 mwaka huu.
Aidha Kigaila amesema kuwa umoja huo
hauridhishwi na msimamo wa Serikali wa kupendekeza kura ya maoni kupigwa April 12 na kusema kuwa mpaka siku hiyo uboreshwaji wa dafari utakuwa bado haujakamilika.
Chapisha Maoni