0
Na Felix Mwagara, Nachingwea


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, Mathias Chikawe ametangaza rasmi kuwa atagombea tena katika nafasi ya ubunge kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu ujao na kulitetea jimbo lake. 

Alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa CCM wa Wilaya na Kata ya Mtua, wilayani Nachingwea katika sherehe ya kuwapokea
viongozi na wanachama wapya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliojiunga na CCM wilayani humo.

Waziri Chikawe alisema wananchi wake
bado wanamuhitaji kwa hiyo hawezi
kuacha kugombea nafasi hiyo kwani wazee na wananchi mbalimbali katika Kata zote alizokuwa akipita kufanya mazungumzo nao wanamuomba agombee tena nafasi
hiyo.
“Wakati nikiingia ubunge mwaka 2005
katika jimbo hili kulikuwa hakuna lami na barabara nyingi za kwenda vijijini zilikuwa hazipitiki na pia maji yalikuwa shida lakini
sasa barabara za lami mjini Nachingwea
zimejengwa, maji yanapatikana tena yasio na chumvi, barabara vijijini zinapitika kwa kuwa zimechongwa vizuri kwa kuwawezesha wakulima kupitisha mazao yao,” alisema Chikawe huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliofurika katika sherehe hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top