0
Waandamaji wenye hasira nchini Burkina Faso wamelichoma moto jengo la bunge kufuatia mipango ya Rais Blaise Compaore kutaka
kurefusha kipindi chake cha utawala uliodumu kwa miaka 27.

Mamia ya watu walivuka ulinzi mkali katika jengo la bunge katika mji mkuu Ouagadougou, ambapo walichoma moto magari kabla ya kukivamia kituo
cha runinga cha serikali na kisha ikulu.

Mtu mmoja aliuawa katika vurugu hizo zilizozuka muda mfupi kabla ya wabunge kupigia kura sheria
ambayo ingemwezesha Compaore — aliyeingia madarakani mwaka 1987 kwa mapinduzi kugombea tena nafasi hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top