CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) kimesema kinaingia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bila kuungana na
chama chochote cha siasa kwa sababu
wanaamini itikadi za vyama hivyo haiendani na itikadi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Mawasiliano na Uenezi Taifa, Karama Kaila alisema ACT haijaungana katika muunganiko wowote na vyama vingine kama ilivyo kwa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na taarifa za kwamba nao wako katika muungano huo ni upotoshaji.
“Kuna taarifa zimezagaa katika mitandao ya kijamii kwamba na sisi tupo katika hiyo muungano wao, sisi hatujaungana na chama chochote na tunaingia katika uchaguzi wa Serikali
za mitaa tukisimama wenyewe,” alisema.
Aidha, alisema ACT itaweza kuingia katika muungano wa kisiasa endapo tu muungano huo utakuwa ni wa kiitikadi na kifalsafa lakini katika muungano uliopo ukiwamo ule wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) hauna mrengo unaofanana na ACT.
Mwenyekiti wa ACT mkoa wa Dar es Salaam, Hamisi Chambuso alisema katika mkoa huo chama mpaka sasa kina wagombea 56 katika wilaya ya Temeke, 32 Kinondoni na Ilala 19 na
kwamba ACT itakuwa na wagombea karibu nchi nzima katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ingawa alisema kwamba kwa Mkoa wa Pwani
hawana imani nao.
Chapisha Maoni