0
Mkuu wa sheria nchini Mexico anasema kuwa genge moja la wahalifu limekiri kuwaua zaidi ya wanafunzi 40 ambao walitoweka wiki kadha zilizopita.

Jesus Murillo alisema kuwa wanachama wa genge la madawa ya kulevya la Guerreros Unidos linasema kuwa liliwaua wanafunzi hao na kisha
likachoma maiti zao.

Kundi hilo lilisema kuwa lilikabidhiwa wanafunzi hao na polisi baada ya makabiliano kwenye mji wa
Iguala.
Mkuu huyo wa sheria anasema kuwa mabaki ya maiti hizo yamepatikana kando ya mto na uchuguzi wa DNA utafanyika nchini Austria ili kuitambua.

Familia za wanafunzi hao zinasema kuwa zinaamini kuwa wanafunzi hao bado wako hai. Meya wa mji wa Iguala yuko kizuizini kufuatia kuwaamrisha polisi kuingilia kati ili kuwazuia
wanafunzi hao kuandamana.

Chapisha Maoni

 
Top