0
Shirika la madaktari wasio na mipaka Medecins
Sans Frontieres limesema kuwa viwango vya Ebola nchini Liberia humo vimeshuka kidogo.

Hata hivyo shirika hilo limeonya kuwa kuna ongezeko la visa vya ugonjwa huo nchini Guinea na Sierra Leone likisema kuwa visa vya maambukizi vilivyokuwa vimepungua nchini Guinea vimeongezeka tena.

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa mafanikio nchini Liberia yanatokana na jitihada za kuzika maiti kwa njia iliyo salama.
WHO inasema kuwa karibu watu 5000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo.

Chapisha Maoni

 
Top