0
Hatimaye mpenzi wa sasa (Wema) na mpenzi wa zamani (Penny) wa msanii wa Bongo fleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz wamemaliza
tofauti zao zilizotokana na ‘penzi’ la hit makerbhuyo wa ‘Number 1’.

Muigizaji wa Bongo Movie Wema Sepetu na mtangazaji wa E-FM Penny Mungilwa a.k.a VJ Penny walikutana usiku wa jana kwenye birthday dinner ya rafiki yao aitwaye Junaithar ambaye ndiye aliyewapatanisha.

Picha za Wema na Penny wakikumbatiana huku nyuso zao zikiwa na tabasamu zimeashiria kuwa
sasa kila mmoja ameacha yaliyopita na hana kinyongo na mwenzake.

Kupitia Instagram Junaithar aliyewapatanisha aliandika:
“Wema na penny leo wamemaliza tofauti zao nilijuwa wema kupitaa penny nawapenda sana wadogo zangu 

@wemasepetu_auntyezekiel
@vjpenny04 @nsepetu”

Chapisha Maoni

 
Top