Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi,
Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa
tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya
Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la
Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo
baada ya madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa
Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina
hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na
kuchukua kiasi cha saa moja unusu,
umefanyika salama na kwa mafanikio
makubwa.
Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete
inaendelea vizuri, bado yuko wodini
akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa
madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea kupewa taarifa
sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete kwa
kadri zitakavyokuwa zinapatikana.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS,
IKULU DAR ES SALAAM, NOVEMBA 9, 2014
Chapisha Maoni