0
Mamlaka kusini mwa Somali inasema kuwa zaidi
ya wapiganaji 70 wa kundi la Alshabaab waliuawa katika mapigano siku ya jumamosi katika vita vya kukidhibiti kisiwa muhimu cha kudha.

Alshabaab limechukua udhibiti wa kisiwa hicho ,na linasema kuwa limewaua zaidi ya wanachama 60 wa jeshi moja la afrika mashariki,linasaidia serikali ya Somali.

Mamlaka katika jimbo la Juba nchini Somali imewashtumu wanachama wa Al shabaab kwa kuwaua raia.
Vikosi vya wanajeshi wa Afrika pamoja na wale wa Somali katika miezi ya hivi karibuni vimehusika katika kuwafurusha wanamgambo hao kutoka miji
kadhaa na vijiji kusini mwa Somali.

Chapisha Maoni

 
Top