0
 Simba Sports Club wamefanikiwa
kupata ushindi wao wa kwanza kwenye ligi ya soka Tanznaia bara baada ya kuwafunga Ruvu Shooting.

Najua mashabiki wengi wa Simba walikua wanasikilizia sana hii mechi ya leo kama ilivyoahidiwa na club hiyo na kweli kitu kikajibu ambapo mpaka Full Time ilikua Simba 1 – 0 Ruvu Shooting.

Bao pekee lililoipa Simba ushindi lilifungwa na mchezaji wa kimataifa toka Uganda Emmanuel Okwi ambaye alifunga bao hilo kwenye dakika ya
78 ya mchezo huo zikiwa zimesalia dakika 12 tu kabla ya mchezo kumalizika.

Simba walitawala mchezo huo tangu mwanzo hadi mwisho wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga ambazo hata hivyo walishidnwa kuzitumia huku washambuliaji wake wakikosa
umakini walipokuwa wakifika langoni.
Ruvu Shooting nao walijitahidi kuleta presha langoni mwa Simba lakini walishindwa kabisa kufanya kile ambacho timu tano zilizocheza na
Simba kabla ya mchezo huu wa leo zimeweza kukifanya, yani kuifunga.

Ushindi huu unawafanya Simba kufikisha pointi tisa baada ya kushinda mchezo mmoja huku wakitoka sare sita na wanapanda toka nafasi ya kumi mpaka nafasi ya sita.

Matokeo haya pia yanamaanisha kuwa Simba wanaendelea kuwa moja kati ya timu mbili ambazo hadi sasa hazijaweza kupoteza mchezo wowote huku timu nyingine ikiwa Mtibwa Sugar.

Chapisha Maoni

 
Top