Hoteli hiyo inatoa huduma kama vile vidimbwi vya kuoga vya wanyama hao,vyumba vyenye hewa safibna vyakula vya kuvutia, na hivyobasi kuimarisha
viwango vya kuwabembeleza wanyama hao katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa.
Hoteli hiyo yenye urefu wa futi 4,317 kwa jina Wagington Hotel imejengwa katika nyumba za zamani za wakolini wa Uingereza zilizobadilishwa katika makaazi ya wanadiplomasia.
Vyumba vya kulalia katika hoteli hiyo vinagharimu dola 271 kwa mbwa watatu wanaotumia kwa pamoja chumba cha kifalme,kilicho na maeneo ya kifahari ya kuweka balbu,runinga,na vitanda
vilivyotengezwa na ngozi.
Hoteli hiyo iliojengwa hususan kwa mbwa pia huwakaribisha paka.
''iwapo tunajitakia mema katika maisha yetu, kwa nini marafiki zetu walio waaminifu nao tusiwafanyie mambo mazuri'' aliuliza mmiliki wa hoteli hiyo
Estelle Taylor.
''Kama watu tunaowapenda wanyama,tuna hisi
kwamba ni vyema kuwa na eneo ambalo wanyama wanaweza kuwekwa ili nao wajisikie nyumbani'' aliongezea.
Wanaomiliki wanyama hao pia wanaweza kupata eneo la kufanya mafunzo,kunyoa, kukata kucha,kubadilisha rangi za wanyama hao pamoja na masaji.
Hoteli hiyo pia hutoa huduma ya gari la kifahari aina ya Limousine kwa wanyama hao kutoka makaazi yao hadi hoteli hiyo na kutoka hoteli hiyo
hadi makaazi yao.
Nchini Singapore kuna zaidi ya maduka 250 ya wanyama, mengi yakiwa katika maduka makubwa ya jumla.
Mfanyibiashara mmoja hutoa huduma za kitalii kila wikendi ambapo wamiliki wa wanyama hao na wanyama wenyewe hutembezwa katika maboti.
Chapisha Maoni