0
Programu ya kuwaunganisha mashoga nchini Uchina imejipatia ufadhili wa dola millioni 30 kutoka kwa wawekezaji wa kampuni ya DCM.

Blued, iliobuniwa na mtandao wa jamii wa Danlan mwaka 2012 hutumiwa na takriban watu millioni 15.

Kulingana na mtandao wa habari wa Tech barani Asia,watumiaji hao wanaonekana kutoka katika miji mikuu mikubwa kama vile,Beijing,Shangai na
Guangzou.
Ushoga nchini Uchina ulikuwa haramu hadi mwaka 1997 na ulionekana kama ugonjwa wa akili hadi mwaka 2001.
Xiaofeng Wang ,ambaye ni mchambuzi katika kampuni ya utafiti ya Forrester ,amesema katika ripoti ya kampuni hiyo ya huduma za data kwamba programu za mesenja zina umaarufu mkubwa nchini Uchina kwa kuwa kasi ya mtandao wa simu iko chini.

Lakini katika kuchumbiana, programu hiyo hutumika wazi na wapenzi wa jinsia
tofauti,programu moja ya kuchumbiana kwa jina Momo ina takriban watumiaji millioni 52.
Lakini upande wa mashoga swala hilo hufanywa kwa siri kubwa sana.''Huwezi kuwaona mashoga walio na ari ya kutangaza jinsia zao''.alisema
Forrester.

Nchini Uchina takwimu rasmi zinaripoti kwamba kuna wavulana 118 kwa kila wasichana 100 wanaozaliwa katika famila za wachina.

Chapisha Maoni

 
Top