Tanzania, Mheshimiwa Profesa Jakaya
Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za
Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa
Dkt. Fenella Mukangara kuomboleza kifo
cha Mwanamuziki Muasisi wa Bendi
Maarufu ya Twanga Pepeta, na baadaye
Kiongozi wa Bendi ya Ruvu Star, Khamisi
Kayumbu maarufu kama Amigolas
(pichani).
“Nimehuzunishwa na kusikitishwa
na taarifa za kifo cha Mwanamuziki
Khamisi Kayumbu kilichotokea tarehe 9
Novemba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Rais Kikwete amesema
anatambua mchango mkubwa wa
Marehemu Amigolas, katika kuhamasisha maendeleo ya nchi yetu, kupitia sanaa ya
muziki katika kuwafikishia wananchi
ujumbe muhimu wa masuala mbalimbali
ya kijamii na kiuchumi. Amesema kuwa
Hayati Kayumbu alikuwa mfano unaofaa
kuigwa na Wasanii wengine kote nchini.
“Kutokana na msiba huu, naomba
upokee Salamu zangu za Rambirambi kwa kumpoteza mmoja wa Wanamuziki Mahiri hapa nchini, na Rambirambi hizi ziwafikie pia Wanamuziki wengine kote nchini kwa kumpoteza mwenzao”.
Aidha, Rais Kikwete amemwomba
Dkt. Fenella Mukangara kumfikishia
Salamu zake za Pole kwa Familia ya
Marehemu Khamisi Kayumbu kwa
kupotelewa na Kiongozi na Mhimili
madhubuti wa Familia.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Novemba,2014
Chapisha Maoni