MSHAMBULIAJI Mario Balotelli ameitwa kwabmara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Italia chini ya kocha mpya, Antonio Conte.
Mchezaji huyo wa Liverpool amekuwa hana mwanzo mzuri katika klabu yake hiyo mpya, baada ya kufunga mabao mawili tu tangu asajiliwe kwa dau la Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan kutua Anfield - na katika mabao hayo hakuna alilofunga katika Ligi Kuu ya
England.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hajaichezea The Azzurri tangu baada ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City ameichezea mechi 33 Italia na kuifungia mabao 13.
KBalotelli mwenye umri wa miaka 24, mara ya mwisho aliifungia Italia dhidi ya England katika Kombe la Dunia.
Italy itaikaribisha Croatia katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2016 Uwanja wa San Siro Jumapili ya Novemba 16, mwaka huu kabla ya kumenyana na Albania katika mchezo wa
kirafiki Uwanja wa Luigi Ferraris Jumanne ya Novemba 18,.
IKOSI CHA ITALIA;
Makipa: Buffon (Juventus), Sirigu (Paris
Saint-Germain), Perin (Genoa).
Mabeki: Chiellini (Juventus), Moretti
(Torino), Ogbonna (Juventus), Ranocchia
(Inter), Rugani (Empoli).
Viungo: Bertolacci (Genoa), Bonaventura
(Milan), Candreva (Lazio), Cerci (Atletico
Madrid), Darmian (Torino, De Rossi (Roma), De Sciglio (Milan), El Shaarawy (Milan), Marchisio (Juventus), Parolo (Parma), Pasqual (Fiorentina), Soriano (Sampdoria), Verratti (Paris Saint-Germain).
Washambuliaji: Balotelli (Liverpool),
Giovinco (Juventus), Immobile (Borussia
Dortmund), Pellè (Southampton), Zaza
(Sassuolo).
Chapisha Maoni