0
Wakili wa Darren Wilson ambaye ni afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown kwenye eneo la st Louis nchini Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi huyo amejiuzulu.

Mapema wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua ghadhabu miongoni mwa waamerika weusi.

Afisa huyo amekuwa likizoni tangu mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo yalisababisha majuma kadha ya maandamano.

Michael Brown,kijana mweusi nchini Marekani alipigwa risasi na kuuawaGazeti la St Louis limesema kuwa afisa huyo mwenye miaka 28
aliamua kujiuzulu baada ya kitengo chake cha polisi kupokea vitisho kwamba ghasia zitafutia iwapo
ataendelea kuhudumu kama mfanyikazi.

Gazeti hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu ambayo ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi wa idara
ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali hata kidogo. 





Chanzo BBC

Chapisha Maoni

 
Top