0
ENGLAND imewalaza wenyeji Scotland mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa usiku huu.

Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 32 na Wayne Rooney aliyefunga mabao mawili dakika za 47 na 85, wakati bao pekee la wenyeji lilifungwa
na Andrew Robertson dakika ya 83.

Kwa kufunga mabao hayo mawili, Rooney amekuwa mchezaji wa tatu kufunga mabao mengi katika historia ya timu ya taifa ya England kutokana na kufikisha mabao 45, akimpita Jimmy Greaves.

Kikosi cha Scotland kilikuwa: Marshall/Gordon dk46, Whittaker, R Martin, Hanley/May dk66, Robertson, Maloney, Mulgrew, Brown/D Fletcher dk46, Anya/Bannan dk61, C Martin/
Morrison dk46 na Naismith.

England: Forster, Clyne, Cahill/Jagielka dk46, Smalling, Shaw/Gibbs dk66, Oxlade- Chamberlain, Milner, Wilshere/Barkley dk87, Downing/Lallana dk46, Rooney na Welbeck/ Sterling dk46.

Chapisha Maoni

 
Top