0
Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi
ya kuzungumza na mwanamke au
msichana. Kwa njia hii wanaume wengi
wanaishi maisha ya bila kumvutia
mwanamke yeyote.

Hapa kunanjia 15 utakazozitumia wewe
mwanaume ili kuhakikisha humkwazi
mwanamke unayempenda mnapokuwa
katika mazungumzo ;

1. Wakati ukizungumza nae, jaribu
kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu
kumbu yako ya utotoni, matarajio ya
baadae au matamanio yake. Mada hii ya
mazungumzo yenu yatafungua milango
ya hisia zake ghafla.

2. Wanawake huhitaji mwanaume
asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na
kuwaongoza. Wakati unazungumza na
mwanamke tawala mazungumzo yenu na
kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza
kufikiri kuwa nini ulichokuwa
ukizungumzia.

3. Kuwa makini wakati unapokuwa
ukizungumza nae huku akikupatia
majibu yasiyo na hisia zozote za
mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo
kama kwa bahati mbaya uko nae karibu
kiasi cha kugusana, basi jisogeze
pembeni wakati ukiwa unaendelea
kuongea ili asishtukie au unaweza
kumuona hayuko sawa katika utoaji
majibu.. kwa kawaida atakuonyesha
ishara, hivyo kuwa nazo makini.

4. Kumbuka hii kauli mbiu "Ucheshi/
vituko si mapenzi". Wanawake huvutiwa
sana na wanaume wanaoweza kuwafanya
wawe na furaha muda wote. Usijikite
zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi
na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali
jikite zaidi katika mambo yanayomfanya
ajisikie kuwa na msisimko na starehe
wakati ukonae.

5. Zama katika undani wa mazungumzo
baina yako na yeye. Mwanamke
huendana na mwanaume asiyekuwa
muoga wa kuzungumzia mambo binafsi
kwa ukaribu.

6. Wanawake wengi hupenda kujua
maoni yako kuhusiana na jinsi
unavyomuona. Mwambie vitu
unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu
kuwa makini ili usitamke vitu vingine
vitakavyo msababishia apoteze furaha.

7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke,
mwanamke huwa na mashaka na
mwanaume anayempatia vitu vingi kwa
wakati mmoja ama kila mara.
Kwasababu atafikiri vitu unavyompatia
ni kutaka kumvutia tu ili umpate
kiurahisi. Kitu ambacho baadae kitaleta
madhara makubwa.

8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya
kuweza kuongea na mwanamke au
msichana bila kumfanya asikudharau au
kuboreka, basi usitumie njia ya
kumuuliza maswali mengi katika
mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza
mawazo yako kuhusu vitu flani.

9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe umekulia wapi?", uliza "unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.

10. Usifiche utambulisho wako -
zungumza vitu kutoka katika hisia zako,
onyesha uhalisia wako katika
kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu
yeyote.

Njia bora ya kufikiria jinsi ya
kuzungumza na mwanamke, ni
kutambua njia sahihi ya mazungumzo ya
furaha na yakimahaba utakayopenda
kuitumia, isipokuwa usimuige mtu.
Kuzungumza na mwanamke sii vigumu
bali nikujua ni vitu gani hasa mwanamke
hapendi kuvizungumzia na vitu gani
anapenda kuvisikia. Fuata maelekezo
hapo juu utaona matunda yake...kisha
rudi toa maoni yako hapa.

MUHIMU: Maelekezo haya yote
yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye
kuhitaji mapenzi ya kweli - yani sio kwa
wanawake wanaolenga kuchota pesa
kwako na kutokomea. Hivyo kuwa
makini sana

Chapisha Maoni

 
Top