0
UJENZI wa mtambo wa kuchakata gesi asili kwa ajili ya matumizi mbalimbali (LNG) mjini Mtwara unakadiriwa kuchukua miaka takriban saba.

Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Statoil Tanzania Bw. Thomas Mannes amesema kuwa, mambo yakienda kama
yalivyopangwa, mtambo huo utakuwa
tayari kwa uchakataji kati ya mwaka 2022 au 2023.

Akizungumza na viongozi wa dini wa
Tanzania waliotembelea mtambo wa
uchakataji gesi wa Statoil uliopo Karsto,
Bw.Mannes amesema kuwa mradi huo
mkubwa utagharimu mabilioni ya dola za Marekani.

"Tunakadiria itachukua kama miaka saba, mmoja kwa utafiti wa eneo kujua uimara wake kiufundi, miaka miwili ya utafiti wa kiuhandisi na michoro na miaka minne ya ujenzi wenyewe" alisema. 

Kwa mujibu wa
Bw. Mannes,tayari wameishapendekeza
maeneo yanayofaa kwa ujenzi wa mtambo huo na hivi sasa wabia wa mradi wanateua timu ya pamoja itakayosimamia
mradi huo.

Mradi huo utakuwa wa pamoja kati ya
Shirika la Maendeleo ya Mafuta nchini
(TPDC) na kampuni za Statoil, BG,
ExxonMobil, Ophir na Pavilion. Mradi huo
utaenda sambamba na miradi mingine ya mafuta ya vitalu 1,3 na 4 inayoshirikisha TPDC, BG,Ophir na Pavilion na mradi wa gesi wa kitalu 2 wenye ubia kati ya TPDC,
Statoil na ExxonMobil.

Bw. Mannes alieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutakuwa na manufaamakubwa kwa Tanzania kwani kutoongeza mapato na nafsi za ajira, kutachochea biashara za bidhaa na huduma, kutoongeza mchango
katika Pato la Ndani la Taifa (GDP) na
kutaleta uwiano mzuri wa biashara.

Aidha amewataka Watanzania hususani
wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara
kujipanga izuri kwa ajili ya kufanya
biashara ya bidhaa na huduma kwani
kampuni yake itatoa kipaumbele wa
kufanya biashara na wazawa.
Bw. Mannes aliongeza kuwa mkataba kati
ya Statoil na serikali ni wa manufaa kwa
pande zote mbili na kuwa ni wa viwango
na taratibu zote za kimataifa. Naye Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Bw. Ove Tungesvik alisema kuwa mtambo wa Karsto ndio mkubwa kuliko yote barani Ulaya.

Kwa upande wao, viongozi hao wa dini
wameishauri kampuni ya Statoil
kuwajengea uwezo watanzania, kupitia
mafunzo na programu nyingine, kama
Wanorway walivyosaidiwa na wamarekani katika miaka ya 1970, ili watanzania nao waweze kuisimamia sekta ndogo ya mafuta
na gesi katika miaka michache ijayo.

Viongozi hao wa dini wapo mjini Stavanger, nchini Norway katika ziara ya mafunzo ya sekta ndogo ya mafuta na gesi. Ziara hiyo imeandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Serikali ya Norway kupitia kwa Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.

Chapisha Maoni

 
Top