0
 Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Dk. Alex Malasusa akitoa baraka kwa waumina wa kanisa hilo baada ya kumalizika kwa ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
 Askofu Malasusa akiongoza ibada ya Krismasi leo.
Waumini wa Kanisa la Kanisa la Mtakatifu Petro wakiwa katiba ibada ya mkesha wa Sikukuu ya Krismasi. (Picha zote na Francis Dande.)

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Dk. Alex Malasusa amesema kuwa tatizo la ufisadi linaloendelea nchini limechangiwa kwa kiasi
kikubwa na uwoga wa viongozi kusita
kuwachukulia hatua watuhumiwa.

Dk. Malasusa amesyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ibada ya Sikukuu ya Krismas ambayo huadhimishwa kwa kumbukumbu
ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

"Taifa linahitaji viongozi waaminifu na waadilifu kama alivyokuwa Yesu, lakini tofauti ni kwamba lina viongozi wenye asili ya woga na kurushiana, rushiana mpira, sijui nani atakayeweza
kulioko taifa letu, hata hii mnayoiita mihimili mingine haitaweza kuliokoa taifa letu," alisema.

Dk Malasusa aliongeza kuwa jambo
linaloweza kuliokoa taifa ni kila kiongozi
aliyepewa dhamana anatakiwa kuwa mwema na hodari kama alivyokuwa Yesu.

"Viongozi wakiishi kama Yesu katika maisha yao watapata uhodari na ujasiri wa kuchukua maamuzi na ndipo hapo tutapata viongozi wenye huruma, kwa sababu hilo limekosekana katika
jamii yetu kuanzia ngazi ya familia, na ndio sababu nimekuwa nisikia watu wakiiba mamilioni lakini sasa imefikia mabilioni kama ni kweli maswali haya yanatakiwa majibu," alisema.

Dk Malasusa, alisema kuwa kutokana na hali mbaya ya ubadhilifu inayolikumba Taifa hili inaonyesha wazi kuwa Yesu anahitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote ili aweze kulinusuru taifa hili na sio kutegemea uzuri wa sheria zilizopo kuwa mkombozi wa taifa hili.

"Kama uzuri wa sheria tulizo nazo ungekuwa msaada basi tusingeshuhudia magereza zikijaa na vijana wangeweza kuondokana na mateso waliyo nayo, hayo yote hayataweza kufanikiwa kwa uzuri
wa viongozi tulionao na wala si maneno yao mengi wanayotuahidi," alisema.

Dk. Malasusa alisema kuwa sikukuu hiyo itumike kuwabadilisha wanadamu kwa kuishi maisha yanayompendeza Mungu ndiyo itatoa haki ya
kusherehekea sikukuu ya Krismas.
       

                      Africa Newss

Chapisha Maoni

 
Top