Staa wa sinema Bongo, Rose Ndauka
akifurahia jambo.
MASTAA wa sinema waliowahi kuwa
wapenzi enzi hizo, Rose Ndauka na
Single Mtambalike ‘Richie’ wanadaiwa
kurudiana na hivi sasa ni mapenzi
motomoto!Kwa mujibu wa chanzo, Rose
na Richie wamedaiwa kurudiana baada
ya mwanadada huyo kumwagana na
mzazi mwenzake, Malick Bandawe miezi
ya hivi karibuni.
“Hivi nyie wadaku mnajua Rose Ndauka
na Richie sasa hivi ni mahaba niue kama
zamani? Wamekuwa wakigandana na
mara nyingine hupatikana maeneo ya
Bahari Beach (jijini Dar) kiasi kwamba
wasanii wenzao tunawashangaa.
“Inaonekena walipomwagana hakuna
aliyekuwa tayari,” alisema msanii mmoja
wa filamu za Bongo ambaye aliomba jina lake kusokomomezwa kwenye
makabrasha ya gazeti hili.Baada ya
kuzinyaka habari hizo, Amani lilimtafuta
Richie kwa njia ya simu ya mkononi ili
aeleze chochote kuhusu madai hayo.
Staa wa sinema Bongo, Single Mtambalike
‘Richie’ akipozi. “Unaposema tumerudiana una maana
gani? Mimi sijawahi kuwa na uhusiano
na Rose Ndauka itakuwaje sasa
turudiane? Hakuna kitu kama hicho,
mimi na Rose tulikuwa tunacheza filamu
ambayo nilimshirikisha na tumemaliza.
“Halafu sikia wewe, mimi si mtu wa
magazeti na endapo mtaandika hii habari nitamfanyia mtu ‘kitumbaya’ hadharani maana ninyi mnatafuta habari za uongo ili mpate fedha.”
Baada ya Amani kumalizana na Richie,
lilimsaka Rose Ndauka ambaye naye
aliruka kimanga: “Ha! Ha! Mimi
sijarudiana na Richie, tulikuwa tunacheza filamu moja ndiyo maana muda mwingi tulionekana kuwa wote. Lakini filamu yenyewe tumeshamaliza.”
akifurahia jambo.
MASTAA wa sinema waliowahi kuwa
wapenzi enzi hizo, Rose Ndauka na
Single Mtambalike ‘Richie’ wanadaiwa
kurudiana na hivi sasa ni mapenzi
motomoto!Kwa mujibu wa chanzo, Rose
na Richie wamedaiwa kurudiana baada
ya mwanadada huyo kumwagana na
mzazi mwenzake, Malick Bandawe miezi
ya hivi karibuni.
“Hivi nyie wadaku mnajua Rose Ndauka
na Richie sasa hivi ni mahaba niue kama
zamani? Wamekuwa wakigandana na
mara nyingine hupatikana maeneo ya
Bahari Beach (jijini Dar) kiasi kwamba
wasanii wenzao tunawashangaa.
“Inaonekena walipomwagana hakuna
aliyekuwa tayari,” alisema msanii mmoja
wa filamu za Bongo ambaye aliomba jina lake kusokomomezwa kwenye
makabrasha ya gazeti hili.Baada ya
kuzinyaka habari hizo, Amani lilimtafuta
Richie kwa njia ya simu ya mkononi ili
aeleze chochote kuhusu madai hayo.
Staa wa sinema Bongo, Single Mtambalike
‘Richie’ akipozi. “Unaposema tumerudiana una maana
gani? Mimi sijawahi kuwa na uhusiano
na Rose Ndauka itakuwaje sasa
turudiane? Hakuna kitu kama hicho,
mimi na Rose tulikuwa tunacheza filamu
ambayo nilimshirikisha na tumemaliza.
“Halafu sikia wewe, mimi si mtu wa
magazeti na endapo mtaandika hii habari nitamfanyia mtu ‘kitumbaya’ hadharani maana ninyi mnatafuta habari za uongo ili mpate fedha.”
Baada ya Amani kumalizana na Richie,
lilimsaka Rose Ndauka ambaye naye
aliruka kimanga: “Ha! Ha! Mimi
sijarudiana na Richie, tulikuwa tunacheza filamu moja ndiyo maana muda mwingi tulionekana kuwa wote. Lakini filamu yenyewe tumeshamaliza.”
Chapisha Maoni