0
Mh. Stephen Wassira, amekiri kuwa
kutochukua hatua za mapema kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow ni moja ya sababu ambayo imesababisha chama hicho kutofanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mh,Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu ameyasema hayo nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Kijijini Butiama,
ambapo amesema kitendo cha serikali
kushindwa kutoa taarifa kwa wakati
kimechangia kuwachanganya Watanzania kuhusu sakata hilo.

Hata hivyo mjumbe huyo amesema hivi sasa taifa linakabiliwa na wimbi kubwa la baadhi ya viongozi wake kukosa uzalendo na uadilifu huku wakitanguliza mbele maslahi binafsi kitendo ambacho amesema kinaondoa dhana
nzima ya kumuenzi baba wa taifa
Naye mmoja ya watoto wa baba wa Taifa Mh.

Makongoro Nyerere, ametumia mazungumza hayo na Mh. Wassira kuitahadharisha CCM, kuwa endapo itashindwa kudhibiti vitendo vya
rushwa, matumizi mabaya ya fedha katika uchaguzi kuna hatari ya kuwagawa watanzania na kufanya CCM kupoteza dola katika uchaguzi mkuu ujao.

Chapisha Maoni

 
Top