Rais Kikwete ameahirisha kulihutubia taifa kupitia "Wazee wa Dar" ambapo sasa ataongea nao Jumatatu wiki ijayo(Disemba 22, 2014). Ikulu
imethibitisha na kusema muda utatangazwa.
Rais kikwete jana tarehe 19 alitarajiwa kulihutubia taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es salaam katika mkutano wake ambao ulikuwa ufanyike katika ukumbi wa Hotel ya Blue Pearl,Ubungo
jijini Dar es salaam.
Katika mkutano wake huo Rais Kikwete alitazamia kuzungumzia mustakabali wa nchi sambamba na kuweka wazi juu ya sakata la utekelezaji wa maazimio nane likiwamo la Bunge la kuwawajibisha viongozi waliotajwa katika sakata la
uchotwaji wa fedha bilioni 360 katika akaunti ya Tegeta Escrow Pamoja na mambo mengine.
Katika maazimio nane ya bunge
yaliyopendekezwa yalitaka viongozi waliotajwa katika ripoti hiyo kwa tuhuma za uchotwaji wa fedha kuchukuliwa hatua za kinidhamu na hata wanapo bainika kufilisiwa mali zao na kushitakiwabkatika vyombo husika kwa kuonekana kulihujumu taifa katika sakata hilo la uchotwaji wa fedha
akaunti ya Escrow.
Rais pia alipanga kuzungumzia juu ya Sekta ya Elimu pamoja na agizo lake la ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari nchini,Upigaji kura za
maoni kuhusu katiba Mpya utakao fanyika Aprili 30 pamoja na daftari la wapiga kura.
Hata hivyo Katika Hotuba hiyo Rais aliazimia kuelezea uchaguzi wa serikali za Mitaa ulivyo fanyika ambao ulionekana kukumbwa na dosari
kadhaa katika vituo vya kupigia kura katika sehemu mbali mbali za nchi ulipo kuwa ukifanyika uchaguzi huo ambao uliweza kugharimu maisha ya watu .
Chapisha Maoni