alilazimika kulipa faini ya dola elfu ishirini pesa za
Marekani baada ya kutumia maneno yenye matusi
alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko
katika kisiwa cha St Kitts and Nevis.
Fifty cent ambaye anafahamika kwa jina kamili
Curtis Jackson alikuwa amepangiwa kuwa 'Mcee'
katika tamasha hilo la muziki huko Caribbean
lakini alipopanda jukwaani mashabiki walimsihi
awape kionjo cha muziki wake.
Alipokubali 'DJ' alicheza wimbo wake mmoja na
wimbo huo ulikuwa na matusi kochokocho jambo
ambalo ni hatia katika kisiwa hicho kilichotawaliwa
na Uingereza.
50 cent hakufahamu alikuwa amevunja sheria hadi
alipofika katika uwanja wa ndege siku ya Jumapili
akikusudia kuondoka.
Hata hivyo maafisa wa forodhani walimkamata na
kumzuilia hadi jumatatu alipofikishwa mbele ya
hakimu na kusomewa mashtaka yake.
50 cent alikiri makosa yake na kupigwa faini ya
takriban dola 20,000 pesa za marekani kabla ya
kuruhusiwa kuondoka
BBC
Chapisha Maoni