0
Kufuatia kura ya maoni ya Uingereza kujitoa ndani
ya Jumuiya ya Ulaya waziri wa mambo ya kigeni
wa Marekari John Kerry amesema Marekani
inaangalia mfumo wa ushirikiano na Uingereza
kiuchumi.
Msimamo huo wa Marekani dhidi ya Uingereza,ni
kufuatia kura ya maoni ijumaa wiki iliyopita, kujitoa
katika jumuiya ya Ulaya. John Kerry ameyasema
hayo katika mazungumzo na waziri wa mambo ya
nje wa Uingereza Phillip Hammond
Hata hivyo waziri Hammond alitaka kujua kama
Rais Obama anamtazamo tofauti na kauli yake ya
awali,kuhusiana na Uingereza ambapo awali
alisema Uingereza itarudi mstari wa nyuma
kibiashara iwapo itapiga kura kujitoa.Lakini Waziri
Kerry akalitolea ufafanuzi hilo.
John Kerry anasema kilicho salia kwa Marekani ni
kusubiri na kuona matokeo ya mazungumzo hayo
na kuamua ni kwa mfumo gani uendeshaji wa
mahusiano ya kibiashara utakuwa iwapo kutakuwa
na mabadiliko ya kimfumo.
Akizungumzia kauli ya Rais Obama alisema
Uingereza imekuwa na ushirikiano imara na
Marekani kwa miaka mingi,na kuwa rais atafanya
kila linalowezekana kusaidia kwa namna yoyote
kuimarika kwa umoja uliopo na Uingereza na pia
kusaidia jumuiya ya Ulaya kwa maslahi ya usalama
wa dunia na ustawi wa dunia kwa ujumla
BBC

Chapisha Maoni

 
Top