wilayani Magu, Wilson Magola (45), amekufa
baada ya kunywa pombe haramu ya gongo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoani Mwanza, Ahmed
Msangi alisema jana kuwa, tukio hilo lilitokea Juni
23, mwaka huu, saa 8:00 mchana kitongojini
humo.
Msangi alieleza kuwa, baada ya kufika nyumbani
kwa Daudi Mtula anayeuza gongo kwa siri Magola
alikunywa pombe hiyo kupita kiasi akaishiwa
nguvu na kupoteza maisha.
“Mtu huyo pia alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa
wa kifafa,” Kamanda Msangi alisema na kuongeza
kuwa, baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka
na kuuacha mwili wa marehemu nyumbani
kwake.
Alisema kuwa Polisi inamtafuta kwa ajili ya
kumchukulia hatua za kisheria.
“Tulipata taarifa kutoka kwa raia mwema na
tulipofika nyumbani kwa mtuhumiwa tuliupata
mwili na tayari umekwishafanyiwa uchunguzi na
kukabidhiwa kwa familia kwa ajili ya maziko,”
alisema.
Alitoa wito kwa wananchi kuiunga Polisi mkono
kudhibiti biashara ya pombe hiyo haramu.
Chapisha Maoni