0
LIONEL MESSI ametangaza kustaafu
kuichezea Timu ya Taifa ya Argentina mara
baada ya mapema Leo kupaisha Penati
kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano wakati
Argentina ikibwagwa kwa Penati 4-2 na Chile
kwenye Fainali ya Copa America Centenario.
Akiongea baada ya Mechi hiyo Messi alisema:
"Haya hayakupangwa kwangu. Kwangu mimi
Timu ya Taifa imekwisha. Nimefanya kila
niwezalo na inauma sana kutokuwa Bingwa."
Messi, mwenye Miaka 29, alianza kuichezea
Argentina Mwaka 2005 na kucheza Mechi 115
ambapo Juzi alivunja Rekodi ya Ufungaji Bora
Argentina ya Gabriel Batistuta kwa kupachika
Bao 55.
Lakini ukiachia Medali ya Dhahabu ya
Olimpiki aliyotwaa Mwaka 2008, Messi
hajatwaa Taji lolote huku Argentina ikibwagwa
katika Fainali kubwa 4.
Kuanzia 2014, Argentina na Lionel Messi,
Mchezaji Bora Duniani mara 5, wamefika
Fainali 3 na zote kufungwa.
2014 walicheza Fainali ya Kombe la Dunia
huko Brazil na kufungwa na Germany 1-0 na
Mwaka Jana kutolewa kwa Penati na Chile
huko Santiago kwenye Copa America.
Leo Alfajiri huko USA, kwenye Fainali ya Copa
America Centenario, Argentina na Chile
zilitoka 0-0 katika Dakika 120 za Gemu na
Gemu kuamuliwa kwa Mikwaju ya Penati.
Baada ya Chile kukosa Penati ya Kwanza,
Messi akaja kuipigia Argentina Penati yao ya
kwanza na kupaisha.
Argentina wakakosa Penati nyingine na Chile
kushinda kwa Penati 4-2 na kubeba Kombe
la Copa America Centenario.
Messi amekuwa na mafanikio makubwa na
Timu yake ya Spain Barcelona ambayo
ametwaa Ubingwa wa La Liga mara 8 na
kubeba UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 4.
Messi aliongeza: "Ni Fainali 4, nimejaribu. Ni
kitu kikubwa nilichokitaka lakini sikupata sasa
nadhani imekwisha. Ni bora kwa kila Mtu
niondoke. Ni ngumu lakini uamuzi
umefanyika. Sasa sitajaribu tena na sitabadili
uamuzi."
Lakini Kipa wa Argentina ambae pia huchezea
Manchester United, Sergio Romero, ana
matumaini atatafakari uamuzi wake na
kuubadili.
Amesema: "Nadhani aliongea wakati akiwa na
munkari kwani tumeikosa nafasi kubwa.
Nashindwa kuelewa Timu ya Taifa bila Messi
itakuwaje!"

Chapisha Maoni

 
Top