0
STRAIKA wa Southampton Sadio Mane
atapimwa afya yake hii Leo baada ya
Southampton kukubali Dau la Liverpool la
Pauni Milioni 30 kumnunua.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amevutiwa
sana na Mchezaji huyu wa Kimataifa kutoka
Senegal ambae aliiua Liverpool Machi 20 kwa
kufunga Bao 2 wakati Southampton ikitoka
nyuma 2-0 na kuifunga Liverpool 3-2 huko
Saint Mary Stadium.
Dili hii inaingia miongoni mwa Dili kali za
Liverpool pamoja na zile za kulipa Pauni
Milioni 32.5 kumnunua Christian Benteke na
ile ya Pauni Milioni 35 kumnunua Andy
Carroll.
Msimu uliopita, Mane, ambae alihamia
Southamton kutoka Salzburg kwa Pauni
Milioni 10 Miaka Miwili iliyopita, aliifungia
Southampton Bao 11 za Ligi Kuu England
katika Mechi zake 37.
Ujio wa Mane utaongeza nguvu Fowadi ya
Liverpool ambao Mafowadi wao wengine ni
Daniel Sturridge, Divock Origin na Christian
Benteke.
Mane anafuata mlolongo wa Wachezaji
kadhaa wa Southampton kuhamia Liverpool
ambapo tangu 2014, Adam Lallana, Dejan
Lovren, Rickie Lambert na Nathaniel Clyne
wote walitua Anfield.
Katika Kipindi hiki, Mane anakuwa Mchezaji
wa Pili kuuzwa na Southampton, ambayo
haina Meneja baada ya Ronald Koeman
kuhamia Everton hivi Juzi, baada ya Mkenya
Victor Wanyama kuhamia Tottenham kwa Dau
la Pauni Milioni 11.

Chapisha Maoni

 
Top