0
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Chidi Benz
amefunguka na kueleza jinsi wadau wa muziki
nchini wanavyosababisha wasanii wa muziki
kuingia kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya.
Chid Benz
Rapper huyo ambaye ameachana na matumizi ya
Madawa ya kulevya hivi karibuni, ameiambia BBC
kuwa wasanii wengi wanaingia kwenye Madawa
ya kulevya baada ya kupata stress za kubaniwa
kwenye muziki.
“Watu wanamsongo wa mawazo, mashabiki wetu
hawajui sisi jinsi tunavyodeal na watu ambao
wanatufikisha kwao, wadau wa muziki, wadau wa
muziki ni watu tofauti sana na wanafanya vitu
vibaya sana,” alisema Chidi. “Wachache wapo
wanaosaidia vizuri, lakini ni wengi wanaoharibu
na wanaharibu sana sana, yaani mtu anakuwa na
kisasi na wewe na yupo tayari kukufanyia kitu
chochote, akushushe, akupinguze mpaka umalize
pesa zote na usipingwe hata wimbo wako
mmoja,”
Pia rapper huyo alisema wasanii wengi
wanabaniwa kutokana na migongano ya
kimaslahi katika kazi au kushare mademu na
wadau wa muziki.
“Huu muziki tunaoufanya na haya maneno
tunayoyaimba, kuna wale ambao wanachukulia
starehe na kuna wengine wanachukulia
unawasema au mabinti zao wanatupenda sisi
wasanii. Unakuta kuna binti amekupenda wewe
msanii, kumbe yule ana mtu mwingine au mdau,
sasa huyo mtu akisikia kwamba Chidi Benz
anadeal na mtu wake, hawezi kuelewa kwamba
mtu wake ndio anamfuata Chidi Benz, ila yeye
atakufanya kitu chochote kile ili akuumize au
akuharibu na ‘akustopishe’ maendeleo yako. Na
inawezekana yule mtu wewe haukudeal naye ila
anakupenda tu kishabiki na anawaambia marafiki
zake hivyo lakini marafiki zake inatokea
wakaibadilisha na wakaiweka kimapenzi, tayari
una vita na mtu wake ambaye anamwangalia,”
alisema Chidi.
Pia rapper huyo amedai kilichomwingiza yeye
kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya ni
kutochezwa kwa ngoma zake kwenye redio na
runinga hali ambayo ilimfanya ajione mpweke

Chapisha Maoni

 
Top