kuwa Uingereza inafaa kujiondoa kwa haraka
katika muungano huo wakidai kuwa kuchelewa
kwake huenda kukazua wasiwasi miongoni mwa
mataifa yaliosalia.
Kamishna wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker
amesema kuwa muungano wa mataifa 27
yaliosalia utaendelea.
Uingereza ilipiga kura ya aslimia 52 dhidi ya 48
kuondoka katika muungano wa Ulaya huku waziri
mkuu David Cameron akisema kuwa atajiuzulu
ifikapo mwezi Oktoba.
Bw Juncker alifanya mkutano wa dharura na rais
wa bunge la Ulaya Martin Schulz ,rais wa baraza la
Ulaya Donald Tusk na waziri mkuu wa Ujerumani
Mark Rutte na kutoa taarifa hiyo siku ya Ijumaa.
Baadaye walitoa taarifa wakisema wanajuta lakini
wanaheshimu uamuzi huo wa Uingereza.
Wameitaka Uingereza kuondoka haraka licha ya
mpango huo kuwaathiri na kwamba kuchelewa
kwake kutazua mgogoro ndani ya muungano huo.
BBC
Chapisha Maoni