0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella
amesema watumishi hewa 367 kati ya 1057
wamebainika kutafuna zaidi ya Sh. bilioni 2
mkoani humo.
Ulipaji wa mishahara watumishi hewa unadaiwa
kufanywa na baadhi ya wakuu wa idara na wakuu
wa vitengo wasiokuwa waaminifu huku wengine
wakituhumiwa kupokea fedha zilizokuwa
zikitolewa.
Mkuu wa mkoa John Mongella ameyasema hayo
mbele ya Susan Mlawi, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi
ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma wakati
wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma.
Mongella amesema, kumekuwepo na baadhi ya
wakuu wa idara na wakuu wa vitengo mkoani
humo wasiokuwa waaminifu ambao
wamesababisha kuendelea kuwepo kwa watumishi
hewa, kitendo ambacho alidai hakitafumbiwa
macho.
Amesema kuwa, katika uhakiki wa watumishi hewa
katika mkoa huo, ulioanza Aprili 18 na kumalizika
Juni 3 mwaka huu, umefanikiwa kuwapata
watumishi hao hewa huku wengine wakiendelea
kulipwa mishahara.
“Kuna watumishi wa 13 katika Halmashauri ya Jiji
la Mwanza na Halmashauri ya Kwimba ambao
wamekopa mikopo benki na wakati hawapo katika
utumishi wa umma na wanaofanya hayo ni wakuu
wa idara.
“Pia kuna watumishi 72 ambao wamelipwa
mapunjo ya mishahara katika halmashari ya Wilaya
ya Magu kupitia akaunti zao za benki na vilevile
wakalipwa tena kupitia dirishani (Double payment)
na kila mmoja alikuwa analipwa zaidi ya milioni
tatu,” amesema Mongela.
Mongela amesema, kutona na kuwepo kwa
watumishi hao, ofisi yake inakusudia kuwafuta
watumishi wote wasiojulikana kwa waajiri,
kuwafuta kwenye malipo watumishi waliofariki,
walioacha kazi waliofukuzwa kazi na waliostaafu.
Wengine watakaofutwa ni waliogombea nafasi
tofauti ikiwemo ubunge, kuwachukulia hatua
maofisa wa halmashauri waliohusika kuanzisha na
kuidhinisha mikopo kwa watumishi waliotoka
katika utumishi wa umma.
Hatua nyingine zitakazochukuliwa ni kuhakikisha
watumishi waliolipwa mapunjo ya fedha za
mishahara zaidi ya stahili zao zinarejeshwa,
kuwachunguza na kubaini maafisa na wasimamizi
wa watumishi waliosababisha upotevu wa fedha
kupitia malipo ya mshahara wa watumishi hewa.
Hata hivyo Mongella amesema, Februari mwaka
huu watumishi hewa waliolipwa mshahara katika
sekretarieti ya mkoa na halmashauri walikuwa
28,068, halmashauri 27, 416 na katika sekretarieti
ya mkoa walikuwa 652 huku watumishi wa
halmashauri waliohakikiwa ni 26, 359 ambao
hawakufika kuhakikiwa ni 1,057.
Na kwamba licha ya kutolewa kwa tangazo la
kuwaita watumishi wote, waliopo masomoni, likizo
na waliohama vituo vyao vya kazi lakini wengine
hawakuweza kutekeleza agizo hilo jambo ambalo
linaonesha wazi ni watumishi hewa.

Chapisha Maoni

 
Top