kuboresha usalama wa raia uliofanyika katika
viwanja vya Biafra amelitaka jeshi la polisi
kuhakikisha linasimamia vyema na kuhakikisha
hakuna mtu ambaye atachelewesha serikali katika
kutimiza mipango yake.
Rais Magufuli alisema kuwa sasa ni wakati wa
kutekeleza mambo ambayo waliahidi kwa
wananchi ili watu waje kumpima baada ya miaka
mitano ya uongozi kama ametekeleza au laa.
Hivyo huu ni muda wa Serikali kufanya kazi yake
pamoja na viongozi mbalimbali ambao wamepewa
ridhaa na wananchi kufanya kazi zao. Ametaka
asitokee mtu mmoja kumchelewesha mwingine.
"Mimi nataka nijenge reli, nataka wa kina mama
waishi maisha mazuri, nataka nitatue changamoto
ya maji katika mji wa Dar es salaam, nataka
kujenga viwanda ili watanzania wapate ajira
mbalimbali, hivyo sitegemei mtu mwingine aje
kunichelewesha kutekeleza haya niliyoahidi kwa
wananchi," amesema Rais Magufuli
"Jeshi la Polisi simamieni jambo hili ili watu
wasitucheleweshe kutekeleza yale tuliyoahidi kwa
wananchi"
EATV
Chapisha Maoni