Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amefunguka kwa
kinywa chake kuwa penzi la mwanamuziki mkali
wa Bongo Fleva, Ali Salehe Kiba ‘Alikiba’ lilitaka
kutoa uhai wake kwani hakuna mwanaume
aliyemshika mtima wake zaidi yake.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Sabby
anayedai ana historia ya kutendwa na wanaume
alisema kuwa amewahi ‘kudate’ na wanaume
wapatao saba lakini kati yao hakuna
aliyemdatisha zaidi ya Kiba ila jamaa huyo alitaka
kusababisha ajitoe uhai.
“Jamani haya mapenzi yaacheni hivihivi, huwezi
kuamini Alikiba alitaka kuniua kwa penzi lake,
nilimpenda sana na alinidatisha kiasi kwamba
nilipokuwa nikihisi ananisaliti, niliumia roho na
wakati mwingine kupata presha.
“Achilia mbali hilo, kuna wakati nilitaka kujiua
kwa sababu yake maana kuna kitu kilitokea,
nikaumia sana hadi nikahisi sina umuhimu wa
kuishi,” alisema mdada huyo.
Inadaiwa Sabby na Kiba waliwahi kuwa wapenzi
kwa siri na haikuchukua muda mrefu
wakamwagana kwa sababu ambazo wanazijua
wenyewe.
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Kiba
angalau agusie kidogo uhusiano wake na binti
huyo ulivyokuwa lakini hakuweza kupatikana
mara moja.
Chapisha Maoni