0
Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
wameanza kudhibiti vitendo vya mauaji kwa
kupitia wapangaji na wenye nyumba
kulazimika kuingia mikataba itakayoambatana
na picha ya mpangaji.
Wamewataka wenye nyumba wanapotengeneza
mikataba waweke picha za wapangaji wao na
nakala zipelekwe kwenye ofisi za Serikali za
mitaa kwa ajili ya usalama.
Hatua hiyo imekuja baada ya jeshi hilo kubaini
kuwa kila linapokwenda kuwakamata
watuhumiwa wanakoishi linakosa taarifa kamili
kutoka kwa wenye nyumba wao.
Kamanda wa Kanda hiyo, Simon Sirro alisema
jana kuwa utafiti unaonyesha wanapowafuatilia
watuhumiwa, wengi wao huwa wamechukua
chumba kimoja ambacho hukaa miezi miwili
hadi mitatu na baadaye wanahamia kwenye
nyumba nyingine.

Chapisha Maoni

 
Top