0
Mchezaji wa zamani wa Manchester United na
England Paul Scholes amesaini mkataba wa miaka
mitatu kucheza kwenye ligi ya Premier Futsal
nchini India. Mchezaji huyu wa Man United
amatajwa kuwa mmoja wa nyota watakaocheza
ligi hiyo pamoja na Deco.
Huu utakuwa msimu wa kwanza wa ligi hii mpya
ambayo itahusisha kuchezwa kwa aina ya mchezo
wa mpira wenye sheria tofauti .
Mchezo huu unachezwa na wachezaji watano
pekee kwa kila timu pia utumia mpira mdogo
zaidi, unaodunda zaidi na unachezwa ndani na si
uwanjani kama ilivyozoeleka.
“Futsal ni mchezo unaofurahisha, na umetoa
mchango mkubwa sana katika kukuza vipaji vya
wachezaji wakubwa zaidi kuwahi kutokea,”
alisema Scholes.
“Premier Futsal ni njia nzuri sana ya kutambulisha
mchezo wa mpira India, na nasubiri kwa hamu
sana kupata nafasi ya kuwasilimia mashabiki wote
nchini India ambao najua ni kati ya mashabiki
bora zaidi duniani.”
Mchezaji wa zamani wa Barcelona Deco na
wachezaji mbalimbali wengine wa mchezo wa
Futsal wameshasaini mkataba kucheza ligi hii na
waandaji wa ligi hii wameahidi kwamba majina
mengine makubwa lukuki yatajiunga na ligi hii
hivi punde.
“Tangu tuzindue ligi yetu tulisema kwamba tunatia
jitihada kuleta vipaji mbalimbali nchini India na
kama inavyonekana kweli tunatimiza ahadi yetu.”
Scholes 41, alifanikiwa kushinda ubingwa wa Ligi
mara 11 na klabu ya Manchester United pamoja
na ligi ya mabingwa 2 akiwa klabu ya Manchester
United kabla ya kustaafu mwaka 2013.
Raisi wa Ligi hii ni Luis Figo mchezaji wa zamani
wa Real Madrid na Barcelona.

Chapisha Maoni

 
Top