Michuano ya Euro mwaka 2016 inaendelea leo
katika hatua ya mtoano (16 bora), ambapo
kunafanyika michezo mitatu katika viwanja vitatu
tofauti.
Saa kumi jioni, Poland wanacheza na Uswisi,
Wales na Ireland ya Kaskazini wanachuana saa 1
usiku, wakati Croatia na Ureno wanapambana
vikali saa 4 usiku.
Tukiangazia mchezo kati ya Croatia na Ureno
ambao utachezwa kunako dimba la Stade
Bollaert-Delelis uliopo manispaa ya Lens.
Huu ni mchezo wa kusisimua ambao
unazikutanisha timu ambazo zimeamaliza hatua
ya makundi na rekodi tofauti kabisa. Croatia
walimaliza kama vinara wa kundi D mbele ya
Uhispania, Uturuki na Jamhuri ya Czech pamoja
na kumaliza ubabe wa Uhispania kutofungwa
mechi 14 mfululizo katika michuano ya
Ulaya, wakati Ureno walimaliza nafasi ya tatu
baada ya kutoka sare michezo yote na kuingia
katika hatua hii kama mshindwa bora (best loser),
kwenye kundi lililokuwa na timu za Austria,
Iceland na Hungary.
Kwa upande wa Croatia, leo kiungo wao mahiri
Luka Modric anaweza kurejea baada ya kuukosa
mchezo dhidi ya Ufaransa kutokana na majeraha
ya nyonga yaliyokuwa yakimsumbua.
Kocha Ante Cacic bado hajafanya maamuzi kama
amtumie mshambuliaji Mario Mandzukic au Nikola
Kalinic, ambaye alifunga katika mchezo dhidi ya
Uhispania.
Croatia watakuwa watakuwa na faida ya kuwa na
mapumziko zaidi, lakini mshambulizi Nikola
Kalinic, amekiri kwamba mchezo wa leo
hautakuwa rahisi kutokana na uimara wa
wapinzani wao.
“Pengine tungeweza kupata wapinzani rahisi zaidi
ya Ureno katika hatua hii, lakini inatubidi kucheza
kwa juhudi kama tulivyofanya kwenye hatua ya
makundi, tuna nafasi kubwa ya kusonga mbele.
Sisi ni moja ya timu bora katika michunao hii, na
kwa uwezo mkubwa wa safu yetu ya kiungo, basi
tuna nafasi kubwa ya kuibiuka na ushindi,” Kalinic
amesema.
“Hii ni fursa adhimu kwa kizazi chetu katika
historia ya taifa letu, na tutakumbukwa tu endapo
tutafanya jambo kubwa hapa,” mshambuliaji huyo
wa Fiorentina ameongeza.
Kocha wa Ureno Fernando Santos amesema
kwamba kikosi chake kipo kamili na wachezaji
wake wote wamefanya mazoezi jana tayari kwa
mchezo wa leo.
Santos anaamini kwamba magoli mawili
ya Cristiano Ronaldo katika mchezo dhidi ya
Hungary Cristiano Ronaldo yatamuongezea
kujiamini, vile vile amesisitiza kurekebisha
mapungufu kwenye safu yake ya ulinzi
yaliyosababisha kuruhusu magoli mengi katika
mchezo uliopita.
“Katika hatua hii hakuna tena nafasi ya kufanya
makosa ya kizembe. Lazima tuwe na uwiano
mzuri kuanzia safu ya ulinzi mpaka ushambulaiji
kwa sababu tunapokwenda kushambullia
tunaancha mapengo mengi nyuma kama
ulivyoona kwenye michezo yetu ya hatua ya
makundi.” amesema Santos.
Beki wa kushoto Raphael Guerreiro amepona
majeraha yake ya misuli yaliyokuwa
yanamsumbua ambayo yalisababisha akose
mchezo dhidi ya Hungary.
Rekodi ya mechi walizokutana
Ureno wameshinda michezo yao yote
mitatu iliyopita dhidi ya Croatia, wakifunga
jumla ya magoli sita na kutoruhusu hata goli
moja.
Katika michuano mikubwa, wamekutana
mara moja tu mwaka 1996. Ureno walishinda
magoli 3-0 katika mchezo wa makundi
kwenye uwanja wa City Ground
uliopo Nottingham (hata hivyo Croatia
walikuwa wameshafuzu kwenda robo fainali,
Ureno pia walisonga mbele).
Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana
ilikuwa ni katika mchezo wa kirafiki June 2013
jijini Geneva nchini Uswisi ambapo goli pekee
la Cristiano Ronaldo liliwapa ushindi Ureno.
Croatia
Croatia wamepoteza mchezo mmoja kati ya
10 iliyopita katika michunao ya Ulaya (ushindi
mara sita, sare mara tatu), huku mchezo wa
robo fainali dhidi ya Uturuki mwaka 2008
ukihesabiwa sare kutokana na kufungwa kwa
penati.
Vile vile hawajafungwa kwenye michezo yao
ya mwisho 10 ya kimataifa. Ikiwa ni michezo
mingi zaidi ya timu yoyote katika michuano ya
Euro mwaka huu.
Katika mashindano makubwa duniani
ambayo Croatia wamewahi kushinda kwenye
hatua ya makundi ilikuwa kwenye fainali za
Kombe la Dunia, wakati waliposhinda michezo
mitatu na kumaliza nafasi ya tatu. Hawajawahi
kushinda mchezo wowote wa mtoano katika
Michuano ya Ulaya. (kufunga mara moja, sare
mara moja)
Croatia wana rekodi ya kucheza katika
uwanja huu wa Stade Bollaert-Delelis.
Walicheza dhidi ya Jamaica katika fainali za
Kombe la Dunia mwaka 1998 na kushinda
mabao 3-1.
Ivan Perisic amefunga na kutoa pasi za
magoli saba katika michuano mbalimbali
(magoli manne, pasi za magoli tatu). Ni Davor
Suker pekee ndiyo mwenye rekodi bora zaidi
kwa taifa hili (magoli tisa, pasi ya goli 1).
Ureno
Ureno ndiyo timu ya kwanza kutoka sare
mechi zote tatu katika hatua ya makundi
kwenye michuano ya Ulaya (Uefa Euro)
Ureno wamecheza michezo mingi zaidi (31)
katika historia ya Michuano ya Ulaya bila
kushinda ubingwa.
Hawajafungwa kwenye mechi zao 10 za
mwisho za ushindani, wakishinda mara saba.
Katika mechi zao zote saba walizoshinda
katika mfululizo huo, kumekuwa na tofauti ya
goli moja-moja tu.
Magoli yao saba ya mwisho katika
Michuano ya Ulaya yamefungwa na
ama Cristiano Ronaldo (matatu) au Nani
(mawili).
Bado goli moja tu Ronaldo atakuwa amefikia
rekodi ya ufungaji ya Michel Platini mwenye
magoli nane katika michuano hii. Magoli ya
Ronaldo yametokana na michuano minne
wakati Platini alifunga katika mwaka mmoja tu
(1984).
Ronaldo amepiga faulo arobaini katika
michuano mbalimbali ya kimataifa lakini bado
hajafunga hata goli moja.
Magoli yote matatu ya Ureno katika mchezo
dhidi ya Hungary yalifingwa nje ya eneo la
penati. Mara ya mwisho kutokea hivi ilikuwa
ni mwaka 1980.
Chapisha Maoni