ROBO FAINALI za EURO 2016, Mashindano ya
Mataifa ya Ulaya, zinaanza Alhamisi kwa Mechi
moja tu huko Stade Velodrome Mjini Marseille
Nchini France kwa Mechi kati ya Poland na
Portugal.
Timu hizi mbili zimetinga Robo Fainali baada ya
kucheza Dakika 120 kwenye Raundi iliyopita
Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Poland walikwenda sare 1-1 na Switzerland katika
Dakika 90 na dakika za Nyongeza 30 hazikuzaa
Bao na ndipo ikaja Mikwaju ya Penati na Poland
kushinda Penati 5-4.
Nao Portugal walitoka 0-0 na Croatia katika Dakika
90 na zikaongezwa Dakika za Nyongeza 30 na
ndipo Portugal kushinda 1-0 kwa Bao la Dakika ya
117 la Ricardo Quaresma alieanzia Benchi.
Kabla ya hatua hiyo, kwenye Makundi, Poland
walifuzu toka Kundi C wakiwa Nafasi ya Pili w
akiwa nyuma ya Mabingwa wa Dunia Germany
baada ya kushinda Mechi 2, zote 1-0 dhidi ya
Northern Ireland na Ukraine, na Sare ya 0-0 na
Germany.
Kwenye Makundi, Portugal hawakushinda hata
Mechi 1 baada ya kutoka Sare Mechi zao zote 3 za
Kundi F dhidi ya Iceland, Austria na Hungary na
kufuzu wakiwa Nafasi ya 3 kwa kuwa moja ya
Timu 4 zilizosonga kwa Tiketi ya Washindi wa Tatu
Bora.
Kazi kubwa kwa Poland, bila shaka, ni kujaribu
kumzuia Cristiano Ronaldo ambae kwenye Fainali
hizi za EURO 2016 ameweka Rekodi kadhaa.
Wiki iliyopita, Ronaldo aliichezea Portugal Mechi
yake ya 128 na kuwa ndie Mchezaji aliechezea
Mechi nyingi Nchi yak.
Pia, alipocheza Mechi yake ya mwisho ya Kundi
lao, dhidi ya Hungary, Ronaldo aliweka Rekodi ya
kuwa Mchezaji aliecheza Mechi nyingi za Fainali za
EURO, Mechi 17, akiwapiku Beki wa France, Lilian
Thuram, na Kipa wa Netherlands, Edwin van der
Sar.
Pia kwenye Mechi hiyo na Hungary, Ronaldo,
aliefunga Bao 2, aliweka Rekodi nyingine ya kuwa
Mtu pekee aliefunga Magoli katika Fainali 4 za
EURO.
Sasa Ronaldo anahitaji bao 1 tu kumkamata Michel
Platini ambae anaongoza kwa kufunga Bao nyingi
katika Fainali za EURO.
Baada ya kuanza EURO 2016 bila kufunga katika
Mechi 2 za kwanza, Ronaldo alipiga Bao 2 kwenye
Mechi na Hungary na katika Mechi yao ya mwisho,
ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Ronaldo ndie
aliesababisha Bao la ushindi walipoifunga Croatia
1-0 katika Dakika za Nyongeza 30 pale Shuti lake
lilipotemwa na Kipa na Ricardo Quaresma
kutumbukiza Mpira wavuni na kuwaingiza Robo
Fainali.
Bilas haka, Masentahafu wa Poland, Michal Pazdan
na Kamil Glik, watakuwa na kibarua kizito kumkaba
Ronaldo na wenzake wa Portugal, Nani na
Quaresma.
Posted Africa Newss Blogger
Chapisha Maoni