Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya
miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeondoka saa 9.45
alfajiri ya leo Juni 30, 2016 kwa ndege ya Shirika
la Ndege la Ethiopia kwenda Visiwa va Hame-
Shelisheli kwa ajili ya kuwavaa wenyeji katika
mchezo wa marudiano kuwania nafasi ya kufuzu
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.
Serengeti Boys inaondoka na matumaini makubwa
ya kuiondoa Shelisheli katika mbio hizo baada ya
kuvuna ushindi mnono wa mabao 3-0 katika
mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, Jumapili ya Juni 26, 2016. Ili ifuzu,
Serengeti Boys inahitaji kusimama imara katika
matokeo hayo ama kwa kupata sare ya aina
yoyote, kushinda au ikitokea kupoteza, basi
isifungwe zaidi ya mabao 2-0.
Lakini Kocha Mkuu wa vijana hao, Bakari Shime
maarufu kama Mchawi Mweusi kutoka Tanga,
amesema, “Nawaheshimu Shelisheli, lakini vijana
wangu hawawezi kuwapa nafasi hata kidogo
wapinzani wetu. Hapa tulishinda, na kwako
tunakokwenda tunakwenda kushinda. Vijana wangu
wa Serengeti Boys wako vizuri. Nawapenda na wao
wanatupenda makocha wao na viongozi wote wa
TFF.”
Katika mchezo wa Dar es Salaam waliozifumania
nyavu walikuwa Nickson Kibabage, Ibrahim
Abdallah na Ally Hussein ambaye alifunga ambao
kila mmoja amepania kufunga kama kocha akiwapa
nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwa
sababu Mchawi Mweusi amefunga safari hiyo
akiwa na kikosi cha nyota 20 wa timu hiyo
inayolelewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi.
Nyota waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani
Awm Kabwili na Samwel Edward Brazio wakati
mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson
Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson
Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi
Makamba.
Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi
Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Benedictor
Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Yassin Muhidini
Mohamed, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji
wakiwa ni Rashid Mohammed Chambo, Mohammed
Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola, Muhsin
Malima Makame na Enrick Vitalis Nkosi.
Serengeti Boys ambayo haina mdhamini badala
yake ikihudumiwa na TFF yenyewe ilikuwa kambini
tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mechi hizo za
kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi
ya Shelisheli na Afrika Kusini ambayo itapambana
nayo baadaye mwezi ujao.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys
ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano
ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA
(AIFF International Youth Tournament 2016) kabla
ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika
Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika
nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
Posted Africa Newss Blogger
Chapisha Maoni