Arsenal wana uhakika meneja wake Arsene
Wenger, 66, atakataa dau lolote kutoka chama cha
soka cha England, FA, ambacho kinamtaka
achukue nafasi ya Roy Hodgson kuwa meneja wa
England (Sun), Laurent Blanc ambaye ameondoka
PSG wiki hii, pia anatajwa kuwania kazi ya
kuifundisha England (Mirror), vilevile meneja wa
zamani wa Chelsea na Brazil, Luiz Filipe Scolari,
67, pia anataka kufikiriwa kupewa kazi hiyo
ambayo aliikataa miaka kumi iliyopita (Daily Mail),
Tottenham na Leicester ni miongoni mwa timu za
EPL zinazomtaka beki wa Iceland Ragnar
Sigurdsson, 30, anayechezea FC Krasnodar ya
Urusi (Guardian), Pep Guardiola atafahamu siku ya
Ijumaa iwapo Manchester City wamefanikiwa
kumsajili mshambuliaji kutoka Colombia Marlos
Moreno, 19, kutoka Atletico Nacional (Manchester
Evening News), Real Madrid wanataka kumsajili
kiungo wa Ufaransa na Leicester City N’Golo Kante,
25 (Marca), meneja wa Arsenal Arsene Wenger
amekataa kusema kama hatoendelea kutaka
kumsajili mshambuliaji wa Lyon, Alexandre
Lacazette, 25 (Canal+), Raheem Sterling
ameshutumiwa vikali na mashabiki wenye hasira
baada ya kuonesha video ya jumba lake la kifahari
pamoja na sinki maridadi la kuogea, muda mfupi
baada ya kurejea na kikosi cha England baada ya
kutolewa kwenye Euro 2016 (Sun), Ryan Giggs
anakaribia kuondoka Manchester United baada ya
miaka 29. Winga huyo wa zamani, 42, amekataa
kazi ya ukocha wa ngazi ya chini, chini ya meneja
mpya Jose Mourinho (Daily Mail), Liverpool
wamewaambia Crystal Palace watalazimika kulipa
pauni milioni 30 kumsajili Christian Benteke, 25
(Telegraph), Manchester City huenda
wakabadilishana na Everton kwa kuwapa Wilfried
Bony, 27, ili wampate John Stones, 22, na ikiwa
Everton watamuuza Romelu Lukaku (Sun), Real
Madrid huenda wakatoa dau la pauni milioni 75
kumtaka nyota wa Ubelgiji na Chelsea Eden
Hazard, 25, kwa kuwapa Alvaro Morata, 23, pamoja
na pauni milioni 40 juu yake (Mirror), Napoli
huenda wakamsajili mshambuliaji wa Monaco
kutoka Colombia, Radamel Falcao, 30, baada ya
Gonzalo Higuain, 28, kusema anataka kuondoka
(La Gazzetta dello Sport), Chelsea watatupilia mbali
mipango ya kumrejesha Darajani Romelu Lukaku,
23, baada ya kukaribia kukamilisha uhamisho wa
Michy Batshuayi, 22, kutoka Marseille kwa pauni
milioni 33.2 (Daily Star),beki kutoka Slovakia
Martin Skirtel, 31, huenda akakamilisha uhamisho
wake kutoka Liverpool kwenda Fernabahce wiki hii
(AMK Spor), mchezaji wa kimataifa kutoka Japan
Takuma Asano, 21, ameuliziwa na Arsenal
(Express), mshambuliaji wa Uholanzi, Robin van
Persie, 32, huenda akauzwa na Fernabahce, mwaka
mmoja tu baada ya kujiunga nao akitokea
Manchester United (Manchester Evening News),
Newcastle wanakaribia kumsajili Dwight Gayle, 25,
kutoka Crystal Palace, na Matt Ritchie kutoka
Bournemouth. Winga Andros Townsend, 24,
ataondoka St James’ Park, huku Crystal Palace
wakitaka kutoa Pauni milioni 13 kumsajili (Daily
Star).
Posted Africa Newss Blogger
Chapisha Maoni