POLISI mkoani Tanga imewaua watu watatu katika
mapigano ya risasi wanaodaiwa kuhusika katika
mauaji ya watu jijini humo wakiwamo watu
wanane waliochinjwa katika Kitongoji cha Kibatini,
Kata ya Mzizima.
Limewahakikishia wananchi kwamba eneo la
Amboni yakiwemo Mapango ya Majimoto
yanayodaiwa kutumiwa na wahalifu
waliosababisha mauaji hasa ya wakazi wanane wa
Kibatini lipo salama, baada ya watuhumiwa
wengine watatu na silaha mbalimbali kukamatwa
juzi.
Waliokamatwa ni Abdulkarim Singano, Seif
Jumanne na Ramadhani Mohamed ambao
baadaye walikufa kutokana na majeraha ya risasi
wakati wa mapigano katika msitu wa Kibatini
wakati askari wakijaribu kuwadhibiti, siku moja
baada ya Abuu Seif anayedaiwa kuwa kiongozi
wao kuuawa jijini Dar es Salaam.
Silaha zilizokamatwa ni bunduki mbili aina ya
SMG, bastola moja, risasi 30, mapanga, majambia
ambavyo vimepatikana kupitia msako
ulioshirikisha kikosi kazi cha vyombo vya ulinzi
na usalama vilivyohusisha askari kutoka majeshi
yote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard
Paulo alibainisha hayo wakati akitoa taarifa ofisini
kwake jana kwamba, wahalifu hao walikamatwa
Juni 28, mwaka huu wakati askari walipokuwa
katika harakati za kuwakamata kwenye msitu wa
Kibatini jirani na mapango ya Majimoto, Kata ya
Mzizima jijini Tanga.
“Majambazi waliohusika kuua wananchi wanane
pale Kibatini ndio tumewakamata lakini kwa bahati
mbaya watatu kati yao wamekufa wakati
wakidhibitiwa na askari,” alisema Kamanda
Paulo.
Alisisitiza wameyakagua yaliyokuwa maficho yao
na kujiridhisha kuwa Amboni iko salama na
imedhibitiwa.
Mapema wiki hii, Polisi wa Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, walitangaza kumuua Abuu Seif
aliyeshiriki katika mauaji ya Tanga, baada ya
kumpiga risasi alipokataa kujisalimisha baada ya
kubainika kujificha katika nyumba moja jijini Dar
es Salaam. Alifariki dunia akipelekwa hospitali.
Related Posts
Tumuombee duwa njema mzee wetu Kig Majuto
Msanii maarufu wa maigizo Amr Athuman ‘King Majuto’ amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimb[...]
Aug 03, 2018Korea kaskazini kuchukua hatua
Korea kaskazini imesema itachukua hatua dhidi ya kutumwa kwa mfumo wa hali ya juu kuzuia [...]
Jul 11, 2016Shilingi bilioni 1.3 zakusanywa daraja la Nyerere
Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimekusanywa kutoka Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar [...]
Jul 11, 2016RAIS MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA INDIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu wa India Na[...]
Jul 10, 2016Jeshi la Polisi Latoa ONYO Kali Kwa Vyama vya Siasa
ONYO limetolewa kwa vyama vya siasavinavyojaribu kusuguana na Jeshi la Polisikukumbuka kuwa hilo n[...]
Jul 10, 2016Haki sawa Wanawake walia Magufuli ‘kuwabania’ katika uteuzi
Mashirika yanayotetea haki za wanawake nausawa wa kijinsi nchini yamesema uteuzi wanafasi muhimu z[...]
Jul 10, 2016
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.