0
Serikali imejikuta katika wakati mgumu wakati wa upitishaji wa Muswada wa Marekebisho ya Sheriy ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016 baada ya
wabunge kupinga baadhi ya hatua zilizochukuliwa
katika muswada huo.
Jana, Bunge lilitumia zaidi ya saa mbili kupitisha muswada huo huku mvutano ukiibuka katika nyongeza ya mapendekezo ya ununuzi wa dawa
na vifaatiba kufanywa kwa dharura na kupinga ka kamati za fedha na mipango kuondolewa katika kusimamia mchakato wa zabuni kwenye
halmashauri.
Mashambulizi hayo yaliongozwa na Mwenyekitw wa Kamati ya Bajeti, Hawa Ghasia na wabunge
Joseph Kakunda (Sikonge CCM), Profesa Anna Tibaijuka (Muleba Kusini CCM) na Andrew Chenge
wa Bariadi Magharibi (CCM), kiasi cha kumfanya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju kukubali baadhi ya mapendekezo ya Bunge kwa shingo upande.
Hii ni mara ya kwanza kwa wabunge wa CCM
kuipinga vikali Serikali kwa kura wakati wa kupitisha vifungu na kufanya Bunge lirudishe uhai
wa mjadala tangu Ukawa waanze kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia
Ackson.
Awali, katika mjadala wabunge wengi walipongeza hatua ya Serikali kupunguza muda na gharama za
mchakato wa zabuni, ushirikishaji wa makundi maalumu katika jamii kwenye zabuni za umma
lakini walipinga uamuzi wa kuwaondoa madiwani katika mchakato wa ununuzi.
Katika kifungu cha 11 cha muswada huo, Serikali
ilikusudia kuondoa jukumu la kamati ya fedha na mipango katika usimamizi wa masuala ya
ununuzi ya halmashauri.
Kabla ya Bunge zima kukaa kama kamati kupitisha muswada huo, Waziri wa Fedha, Dk
Philip Mpango alieleza kuwa Serikali ilikuwa
imeridhia kurudisha jukumu la kamati hizo ambazo huundwa na madiwani kuwasimamia
watendaji watakaoshindwa kutekeleza kazi zao.
Licha ya Serikali kukubali hoja hiyo, wabunge bado waliitaka kuingiza maana katika kifungu cha
pili na kuweka maboresho kifungu cha 24 ili
vifaatiba na dawa vinunuliwe kwa dharura huku Masaju akipinga kwa maelezo kuwa suala hilo
lingeingizwa kwenye kanuni atakazotunga waziri.
Ghasia alieleza kuwa vifaatiba na dawa ni muhimu
katika kuokoa maisha ya binadamu hivyo ni vyema kianzishwe kifungu maalumu katika sheria
badala ya kubaki katika kanuni na kusubiri
majaliwa ya waziri.
Kitendo cha Masaju kupinga pendekezo hilo,
kiliwafanya wabunge, Chenge, Sophia Simba (Viti
Maalumu) na Kangi Lugola wa Mwibara kusimama wakisema Serikali inataka kupitisha mambo
kibabe.
“Kila siku sheria zinakuwa mbaya kwa sababu maoni ya wabunge yanapuuzwa. Serikali ikitaka mambo yake yapite inalazimisha, haiwezekani.
Dawa ni maisha, AG kubali hili na likileta shida mtaleta turekebishe mbona mengine huwa mnaleta tunarekebisha?” alisema Lugola.
Chenge alisema Serikali ingekuwa imeipatia muda kamati ya bajeti imalize kazi zake, kusingetokea
mvutano kwa kuwa mengine wangejadiliana na
kuyamaliza.
Mvutano huo ulimfanya Ghasia kuhamia kwenye meza ya Chenge ili kupata ushauri wa kisheria na
hata wakati mwingine kusahau na kumweleza Naibu Spika kuwa baadhi ya masuala angeeleza
mwanasheria wake (Chenge).
Pamoja na Serikali kukataa mapendekezo hayo,
wabunge walipigia kura ya ‘Ndiyo’ maboresho ya kamati na kuwaacha Masaju na Dk Mpango
wakitikisa vichwa kwa masikitiko.
Hoja nyingine iliyomfanya Masaju kususia kuendelea kutetea ni ile ya Profesa Tibaijuka
iliyopitishwa na wabunge ya kuongeza maneno yatakayowataka wazabuni wa kimataifa kuhusisha
wazawa katika kifungu cha 18 cha muswada.
“Msitunge Sheria kwa hasira. Hiki kifungu kitakuwa kigumu kutekelezeka. Tungeni hivyo lakini mjue itakuja kuleta shida,” alisema Masaju
akionyeshwa kukerwa na kilichofanywa na
wabunge na kueleza maneno hayo tayari
yalikuwapo kwenye Sheria ya Ununuzi ya mwaka
2011 inayoboreshwa.
Sehemu nyingine iliyoleta mjadala ni pendekezl la Kamati ya Bajeti kuongeza kifungu cha kuanzisha akaunti maalumu ya ununuzi mdogo mdogo utakaozisaidia taasisi za umma kutumia
wataalamu wa ndani na kununua vifaa vya marekebisho madogo kama kurekebisha vyoo na
vitasa.
Masaju alipinga pendekezo hilo akisema
litafungua ufisadi katika halmashauri jambo ambalo wabunge wamekuwa wakilalamikia kila
siku.

Chapisha Maoni

 
Top