Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC), imesema imevutiwa na kiungo wa
Yanga, Thabani Kamusoko.
Yanga na TP Mazembe zilichuana juzi
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika
mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka
Afrika (CAF CC) uliomalizika kwa Yanga
kulala bao 1-0.
Akizungumza na gazeti hili juzi baada ya
mchezo huo, Makamu wa Rais wa TP
Mazembe, Mario Kawel alisema
Kamusoko alicheza vizuri na ni aina ya
mchezaji ambaye anafahamu majukumu
yake uwanjani.
Mchezaji pekee wa Yanga aliyemvutia
katika mchezo wa Kombe la Shirikisho
Afrika dhidi yao ni Thabani Kamusoko.
“Mchezaji mzuri aliyenivutia ni yule
mwenye rasta kichwani (Kamusoko), sijui
anaitwa nani, lakini ndiye aliyecheza
kiwango bora katika mchezo wetu, nina
hakika anastahili kucheza kwetu, “
alisema Kawel.
Hata hivyo, alipoulizwa kama watafanya
utaratibu wa kumsajili hivi sasa kwa
kuzungumza na Yanga, alijibu kwa
kuhoji: “Wataka kutusaidia ili iwe rahisi
kumpata?”
Alisema suala la usajili ni mchakato
mrefu, pia linahusisha kwanza klabu na
hatimaye mchezaji kwa kuangalia
maslahi zaidi, hivyo wao wamethibitisha
ubora wake na kwamba kama watataka
wamsajili sasa au baadaye, hilo hawezi
kuzungumza.
“Ni mchezaji wa Yanga, ana mkataba na
Yanga, mimi binafsi nimesema
nimevutiwa naye natamani acheze kwetu,
kwanza nitazungumza na kocha wetu
kuona naye kama amevutiwa, ndipo
tujipange,” alisema kiongozi huyo. Naye
kocha wa TP Mazembe, Mfaransa,
Hubert Velud, alimsifu kiungo huyo na
kusema ana vitu vyote muhimu
anavyopaswa kuwa navyo mchezaji. “Ni
mchezaji mzuri, sijui mkataba wake
ukoje, lakini ningefurahi kujumuika naye
kikosini kwangu,” alisema kocha huyo.
Kamusoko raia wa Zimbabwe, amekuwa
akifanya vizuri katika michuano ya Ligi
Kuu Tanzania Bara na hata michezo ya
kimataifa tangu atue nchini msimu
uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
TP Mazembe ilipokuja kucheza na Simba
mwaka 2011 katika Ligi ya Mabingwa
Afrika na kuibuka na ushindi wa mabao
3-2 iliwasajili wachezaji wa Simba,
mshambuliaji Mbwana Samatta na
kiungo Mganda, Patrick Ochan. Samatta
kwa sasa yupo KRC Genk ya Ubelgiji.
Chapisha Maoni