Uwanja wa Taifa katika mchezo kati ya timu ya
Yanga dhidi ya TP Mazembe na kusababisha
uvunjifu wa mali za uwanja huo, Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) limeahidi kulifanyia kazi suala hilo.
Akizungumza na gazeti hili jana Ofisa Habari wa
TFF, Alfred Lucas alisema kuwa tayari shirikisho
hilo linazo taarifa za kutosha za uharibifu wa mali
za uwanja huo. Alisema kwa sasa anasubiri taarifa
kamili kuhusu gharama za mali zilizoharibiwa ili
kujua ni kiasi gani kitatakiwa kulipwa.
Alisema kuwa anafahamu kuwa mageti pamoja na
mali nyingine za uwanja huo ziliharibiwa na
mashabiki na kuwa ni lazima kuna upande
uwajibishwe kwa hilo.
“ Hili ni suala lisilokubalika kabisa ni suala ambalo
linatakiwa kukemewa na ni lazima wananchi wajue
kuwa uharibifu wa mali na chochote kile uwanjani
hapo sio jambo la kuvumilika,” alisema Lucas.
Aliongeza kuwa, “pindi tukipata habari kamili za
gharama basi ni lazima kuna hatua kali
zitachukuliwa ili iwe ni fundisho kwa watu
wengine.”
Katika mchezo huo wa juzi, Yanga ilifungwa 1-0
na TP Mazembe, ambapo kabla ya kuanza kwa
mchezo huo ambao kiingilio kilikuwa bure
mashabiki wengi walijaa uwanjani hapo.
Baada ya mamlaka husika kuwazuia ndani ya
uwanja huo kufuatia wingi wa watu waliokuwa
wamezidi uwanjani, umati huo ulianzisha vurugu
za kutaka kuingia ndani na hivyo kuvunja mageti.
Polisi ililazimika kutumia nguvu kuwatawanya
mashabiki hao ambao walianza kuingia uwanjani
hapo tangu asubuhi na mapema hali ambayo
ilisababisha kutokea kwa vurugu hizo na kuvunjwa
kwa mageti.
Katika mchezo huo wa kipigo cha 1-0
kumesababisha hali kuwa sio nzuri kwa Yanga
katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho la
Soka Afrika (CAF CC), ambapo hicho ni kipigo cha
pili mfululizo. Juni 19 mwaka huu, ilifungwa na
MO Bejaia ya nchini, Algeria bao 1-0 ugenini.
Chapisha Maoni