amesema bado timu yake ina nafasi ya kufanya
vizuri kwenye mechi zinazofuata na kushika moja
ya nafasi mbili za juu.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara walipoteza mechi
ya pili mfululizo kwenye hatua ya makundi ya
Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika (CAF CC)
baada ya kufungwa bao 1-0 na mabingwa wa
msimu uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika TP
Mazembe.
Awali, wawakilishi hao pekee wa Tanzania kwenye
mashindano ya kimataifa walifungwa bao 1-0 na
Mo Bejaia ya Algeria kwenye mchezo uliopigwa
Bejaia, Algeria wiki moja iliyopita.
“Hatuko nje ya kinyang’anyiro mpaka pale
tutakapokuwa nje. Bado tuna mechi tatu na kila
timu inaweza kufungwa na timu nyingine.
Kama tutafanya vizuri mechi zetu zilizobaki bado
tuna nafasi ya kushika moja ya nafasi mbili za juu,”
alisema Pluijm akizungumzia nafasi ya timu yake
kwenye mashindano hayo.
Pluijm alisema kwamba walifungwa na timu kubwa
yenye uzoefu wa kutosha kwenye mashindano
makubwa, lakini akasema kwamba kama timu yake
ingeweza kutumia nafasi nzuri walizozipata kwenye
kipindi cha kwanza wangeweza kupata matokeo
mazuri kwenye mechi hiyo.
“TP Mazembe walikuwa hatari kwa mashambulizi
ya kushtukiza, lakini tuliweza kuwadhibiti vizuri
kipindi cha kwanza. Kwenye mashindano makubwa
usipotumia nafasi unazopata basi inakuwa rahisi
kwa timu yako kupoteza mechi,” alisema Pluijm.
Pluijm alionesha kufurahishwa na kiwango
kilichooneshwa na chipukizi Juma Mahadhi na
mshambuliaji mpya Mzambia, Obrey Chirwa na
kusema katika mechi yao ya kwanza walionesha
kiwango bora.
Kwa upande wake kocha Mfaransa wa TP
Mazembe, Hubert Velud alisema kwamba walikuwa
bora zaidi ya Yanga ndio sababu walipata matokeo
kwenye mechi hiyo.
“Tulicheza vizuri na kushambulia kwa kushtukiza.
Ulimwengu alicheza vizuri sana na hata bao
tulilopata lilitokana na juhudi zake. Pamoja na
kushinda mwamuzi alitunyima penalti mbili
ambazo ni wazi zilikuwa penalti,” alisema Velud.
Chapisha Maoni