0
SAFU ya Robo Fainali ya UEFA EURO 2016,
Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, imekamilika
Jana baada ya Italy na Iceland kushinda
Mechi zao.
Ifuatayo ni Ripoti kuhusu Timu hizo 8
zilizotinga Robo Fainali inayogusa Rekodi zao
kwenye EURO na pia njia waliyopita kuingia
hatua hii.
RIPOTI YA TIMU 8 ZILIZOINGIA ROBO
FAINALI:
**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za
Bongo
Alhamisi: Poland v Portugal, Marseille
Poland
EURO-Rekodi Bora: Robo Fainali Mwaka 2016
Robo Fainali-Rekodi: Robo Fainali Mwaka
2016
Njia kutua Robo Fainali: 1-0 Northern Ireland,
0-0 Germany, 1-0 Ukraine, 1-1 Switzerland
(Penati 5-4)
Takwimu muhimu: Robert Lewandowski
hajafunga Bao katika Mechi 7 zilizopita
akichezea Poland.
Portugal
EURO-Rekodi Bora: Mshindi wa Pili Mwaka
2004
Robo Fainali-Rekodi: W3 L2
Robo Fainali-Mara yao ya mwisho: 1-0 Czech
Republic, 2012
Njia kutua Robo Fainali: 1-1 Iceland, 0-0
Austria, 3-3 Hungary, 1-0 Croatia
Takwimu muhimu: Cristiano Ronaldo
amebakiza Bao 1 tu kuishika Rekodi ya
Michel Platini ya Ufungaji Bora kwenye Fainali
za EURO akiwa na Bao 9.
Ijumaa: Wales v Belgium, Lille
Wales
EURO-Rekodi Bora: Robo Fainali Mwaka2016
Robo Fainali-Rekodi: Robo Fainali
Mwaka2016
Njia kutua Robo Fainali: 2-1 Slovakia, 1-2
England, 3-0 Russia, 1-0 Northern Ireland
Takwimu muhimu: Wales wametinga Robo
Fainali yao ya kwanza ya Mashindano
makubwa kwa mara ya kwanza tangu Fainali
za Kombe la Dunia za Mwaka 1958.
Belgium
EURO-Rekodi Bora: Mshindi wa Pili Mwaka
1980
Robo Fainali-Rekodi: Mshindi wa Pili Mwaka
1980
Njia kutua Robo Fainali: 0-2 Italy, 3-0
Republic of Ireland, 1-0 Sweden, 4-0 Hungary
Takwimu muhimu: Belgium wamejaribu
Mashuti 84 Golini wakizipta Timu zote
kwenye EURO 2016.
Jumamosi: Germany v Italy, Bordeaux
Germany
EURO-Rekodi Bora: Mabingwa (1972, 1980,
1996)
Robo Fainali-Rekodi: W3 L0
Robo Fainali yao ya mwisho: 4-2 Greece,
2012
Njia kutua Robo Fainali: 2-0 Ukraine, 0-0
Poland, 1-0 Northern Ireland, 3-0 Slovakia
Takwimu muhimu: Chini ya Kocha Joachim
Löw, Germany hawajafungwa hata Bao 1
kwenye Fainali hizi za EURO 2016.
Italy
EURO-Rekodi Bora: Mabingwa (1968)
Robo Fainali-Rekodi: W2 L1
Robo Fainali yao ya mwisho: 0-0 (Walishnda
kwa Penati 4-2) England, 2012
Njia kutua Robo Fainali: 2-0 Belgium, 1-0
Sweden, 0-1 Republic of Ireland, 2-0 Spain
Takwimu muhimu: Italy waliifunga Spain Juzi
kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya
EURO 2016 na kuwa Timu ya kwanza kuitoa
Spain kwenye Raundi za Mtoano za Fainali ya
Mashindano makubwa tangu 2006.
Jumapili: France v Iceland, Saint-Denis
France
EURO-Rekodi Bora: Mabingwa (1984, 2000)
Robo Fainali-Rekodi: W2 L2
Robo Fainali yao ya mwisho: 0-2 Spain, 2012
Njia kutua Robo Fainali: 2-1 Romania, 2-0
Albania, 0-0 Switzerland, 2-1 Republic of
Ireland
Takwimu muhimu: France (1984) ni moja ya
Timu 3 kutwaa EURO wakiwa Wenyeji na
wanaungana na Spain (1964) na Italy (1968)
waliowahi kufanya hivyo.
Iceland
EURO-Rekodi Bora: Robo Fainali Mwaka 2016
Robo Fainali-Rekodi: Robo Fainali Mwaka
2016
Njia kutua Robo Fainali: 1-1 Portugal, 1-1
Hungary, 2-1 Austria, 2-1 England
Takwimu muhimu: Wakiwa na Idadi ya Watu
330,000, Iceland ndio Nchi ndogo kabisa
kucheza Fainali za Mashindano makubwa.

Chapisha Maoni

 
Top