0
Roy Hodgson amejiuzuluzu kama kocha mkuu wa
England baada ya kikosi chake kuchezea kichapo
cha bao 2-1 kutoka kwa Iceland kwenye mchezo
wa hatua ya 16 bora.
Kocha huyo mwenye miaka 68 amekinoa kikosi
cha England kwa miaka minne akichukua nafasi
ya kocha raia wa Italy Fabio Capello lakini
amejikuta akishinda mechi tatu pekee kwenye
mashindano makubwa ya kimataifa.
Iceland taifa lenye wakazi wasiopungua 330,000
ilikuwa ndiyo timu inayopewa nafasi ndogo zaidi
kwenye michuano Ulaya inayoendelea Ufaransa.
“Samahani, inabidi nimalize kwa style hii lakini
tayari yaliyotokea yametokea,” amesema
Hodgson.
“Natumaini bado mtaendelea kuiona timu ya
England kwenye fainali za mashindano makubwa
hivi karibuni”, aliongeza.
“Kwa sasa ni wakati wa mtu mwingine kuja
kuendelea na vijana wenye njaa na wenye vipaji.”
Hodgson ambaye ameshinda mechi 33 kati ya 56
akiwa madarakani, anagekuwa nje ya mkataba
baada ya kumalizika kwa mashondano haya na
inataarifa angeweza kuongezwa mkataba
mwingeine baada ya kufanya mazungumzo na
ma-boss wa FA.
Mwenyekiti wa FA Greg Dyke alishatoa kauli
kwamba, Hodgson angeonezewa mkataba wake
kama tu timu ingefanya vizuri Ufaransa, huku
akisema angalau hatua ya robo fainali lakini
walitakiwa kuifunga Iceland ili kufanikisha hilo.
Kauli iliyotolewa na FA baada ya Hodgson
kujiuzulu, FA imesema: kama taifa
England ilifuzu kucheza Euro 2016 kwa rekodi ya
aina yake. Walianza michuano hiyo kwa sare ya
kufungana goli 1-1 dhidi ya Russia kabla ya
kuichapa Wales 2-1 na kutoka sare ya 0-0
Slovakia kwenye hatua ya makundi na kufanikiwa
kufuzu kwa hatua ya 16 bora.
Chini ya Hodgson kikosi cha England, walifika
hatua ya robo fainali kabla ya kuchezea kichapo
na Italykwenye michuano ya Ulaya iliyopita .

Chapisha Maoni

 
Top