ilifungwa saa tano asubuhi kutokana na wingi
wa mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo na
kuingia moja kwa moja uwanjani.
Hadi kufikia saa 11:53 asubuhi, mashabiki
waliokuwa nje ya uwanja hawakuruhusiwa
kuingia ndani kufuatia majukwaa kufurika
mashabiki, nafasi ya kuingia uwanjani imebaki
kwa watu maalumu na Wanahabari pekee
ambao wanaingilia mlango mkubwa wa Uwanja
wa Taifa wakati ile mingine ikiwa imefungwa.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema
walilazimika kufungua milango ya uwanjani
mapema tofauti na walivyoeleza awali
kutokana na mashabiki kufurika uwanjani
kuanzia saa tatu asubuhi.
"Mashabiki walianza kumiminika uwanjani
kuanzia saa tatu, hatukuwa na namna zaidi ya
kufungua milango ya uwanja muda huo ili
kuwapa fursa ya kuingia na kupunguza
msongamano," alisema Lucas.
Chapisha Maoni