0
SERIKALI imesema shule zote zenye nafasi za
wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwaka
huu, zimejaa hivyo hakuna nafasi ya mwanafunzi
kubadilishiwa shule au mchepuo aliochagua.
Hayo yalibanishwa jana katika taarifa iliyotolewa
jana kwa vyombo vya habari mjini hapa na
Msemaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi), Rebecca Kwandu.
Kwandu alisema baada ya serikali kutangaza
wanafunzi waliojiunga na kidato cha tano, baadhi
ya wazazi na wanafunzi wamekuwa wakifika ofisi
za Tamisemi kuomba kubadilishiwa shule au
tahasusi (michepuo) walizochaguliwa.
“Tunapenda kuwaarifu kwamba shule zote zenye
nafasi za wanafunzi wa kujiunga na kidato cha
tano mwaka 2016 zimejaza, hivyo hakuna
kinachoweza kubadilishwa,” alisema Kwandu.
Aidha, Kwandu alisema vigezo ambavyo
vilitumika katika uchaguzi huo ni pamoja na
ufaulu na uchaguzi wa wanafunzi wenyewe juu ya
masomo wanayopenda kuendelea nayo kidato
cha tano na sita.
“Kulingana na utaratibu uliowekwa na serikali,
mwanafunzi mwenye sifa za kuchaguliwa
kuendelea kidato cha tano na vyuo vya ufundi ni
yule ambaye ufaulu wake ni kuanzia daraja la
kwanza hadi la tatu. Wanafunzi hao wamepangwa
kulingana na ufaulu wao masomo waliyochagua
na nafasi zilizopo, ” alisisitiza.
Pia alisema nafasi za shule walizopangiwa
wanafunzi zimezingatia miundombinu ya shule
husika na uwezo, na kwamba kila shule imepewa
wanafunzi kulingana na nafasi zilizopo, hivyo
hakutakuwa na nafasi ya kuwabadilisha kutoka
shule moja kwenda nyingine kwa sasa.
Kutokana na hali hiyo, aliwataka wanafunzi wote
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na
vyuo vya ufundi kuripoti katika shule na vyuo
walivyopangiwa kama walivyoelekezwa.
Alisema mwanafunzi ambaye hataripoti ifikapo
Julai 24, ambayo ni tarehe ya mwisho kwa muda
uliopangwa, atakuwa amepoteza nafasi yake kwa
kuwa itachukuliwa na mwanafunzi mwingine
ambaye hakupata nafasi awali.

Chapisha Maoni

 
Top